✍️Faraja Gasto
Utangulizi
Uaminifu ni nini?
1. Ni kutokwenda kinyume na mapatano.
2. Ni kutenda sawasawa na maelekezo.
3. Ni kutenda sawasawa na neno lililotamkwa.
Ninaposema Mungu ni mwaminifu maana yake ni kwamba hawezi kufanya jambo lolote nje na agano au nje na neno lake ndio maana Mungu anasema
1. Yeye analitazama neno lake ili alitimize (Yeremia 1:12)
2. Yeye ni Mungu ashikaye maagano (Kutoka 2:24-25)(Zaburi 111:5)
Kila mtu anapaswa kufahamu kuwa Mungu ni mwaminifu katika kuwahudumia watumishi wake kwa huduma mbalimbali, baadhi ya huduma hizo ni kama vile;-
1. Ulinzi.
2. Chakula.
3. Kufariji au kutia moyo.
Unapomtumikia Mungu ni vema ufahamu kuwa Mungu atakuwa mwaminifu katika kukulinda, kukupa chakula, kukutia moyo nakadhalika ENDAPO UTADUMU KUMTUMIKIA KWA UAMINIFU.
HUDUMA YA ULINZI
(Isaya 54:17)(Zaburi 37:28)
Mungu amesema yeye mwenyewe yeye huwa anatoa huduma ya ulinzi Kwa watumishi wake wote, Mungu ndiye bingwa wa kulinda watumishi kwa namna mbalimbali.Ukimtumikia kwa uaminifu, huduma mojawapo utakayopata ni huduma ya ulinzi, ulinzi dhidi ya silaha zote unazozifahamu.
HUDUMA YA CHAKULA
(Zaburi 111:5)
Mungu huwapa watumishi wake chakula kutegemeana na agano lake, Mungu anazo njia nyingi za kulisha watumishi wake.
(Kutoka 23:25)
Huduma mojawapo anayopata kila anayemtumikia Mungu kwa uaminifu ni huduma ya chakula, Mungu atahakikisha unapata chakula, kama una familia Mungu ataleta chakula kwa ajili yako na familia yako ndio maana Daudi aliwahi kusema hajawahi kuona mwenye haki ameachwa Wala watoto wake kuombaomba chakula (Zaburi 37:25
Angalizo: Simaanishi watu waache kufanya Kazi za mikono ila nafundisha kuwa Mungu ni mwaminifu katika kuwalisha watumishi wake kwa njia mbalimbali.
HUDUMA YA KUFARIJIWA AU KUTIWA MOYO
Ukweli ni kwamba kila mtu anahitaji kutiwa moyo au kufarijiwa ndio maana huduma mojawapo ambayo Mungu huwapatia watumishi wake ni kuwatia moyo au kuwafariji ili waendelee mbele wazidi kumtumikia.
(2 Wakorintho 7:6-7)
Zipo njia mbalimbali ambazo Mungu huzitumia kuwafariji au kuwatia moyo watumishi wake, njia mojawapo Mungu huwa anampa mtumishi mtu ambaye atakuwa Faraja kwake Kwa mfano Mungu alimfariji Mtume Paulo kupitia Tito.
(Matendo ya Mitume 2:36)
Mungu aliwafariji mitume na kanisa Kwa ujumla kupitia Yusufu ambaye mitume walimwita Barnaba maana yake "mwana wa faraja"
NB: Mtu ambaye Mungu ameweka ndani yake neno la Faraja, unapokuwa naye huwezi kuchoka kumtumikia Mungu, huwezi kuacha kumtumikia Mungu labda uamue kumuasi Mungu.
NB: Ukitaka kuuona uaminifu wa Mungu, dumu katika kumtumikia kwa uaminifu sawasawa na neno lake na agano lake, fanya Kile ambacho amekuelekeza au atakachokuelekeza bila kujali gharama za hicho alichokuambia yeye atakuhudumia kwa njia mbalimbali na kwa huduma mbalimbali.
Mungu hawezi kusahau uaminifu wako katika utumishi maana yeye ni Mungu mwaminifu.
Ukiumia au kuumizwa wakati uko katika kumtumikia atahakikisha anakuponya maana yeye ni mwaminifu.
Ukipungukiwa nguvu au kuchoka wakati unaendelea kumtumikia Mungu atahakikisha anakupa nguvu mpya kwa kuwa yeye ni Mungu mwaminifu.
Ukipoteza Mali zako nakadhalika wakati unamtumikia Mungu atahakikisha anakurejeshea maradufu maana yeye ni Mungu mwaminifu.
Ukiinukiwa au kushambuliwa wakati unamtumikia Mungu atahakikisha anakupigania kila silaha yoyote itakayofanyika juu yako haitafanikiwa.
0 Maoni