✍️Faraja Gasto
UTANGULIZI
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wake katika nchi ya Tanzania, pia namshukuru Mungu kwa ajili ya kuniwezesha kuandika chapisho hili ambalo naamini litakuwa msaada katika kutoa mchango wa maboresho ya elimu ya msingi na mitaala ya elimu katika nchi yetu ya Tanzania.
LENGO LA CHAPISHO HILI NA HISTORIA FUPI
Mwaka 2015 mataifa wanachama wa umoja wa mataifa yalikutana na yakaafikiana kutimiza malengo 17 ya maendeleo endelevu (17 Sustainable Development Goals) ifikapo mwaka 2030, lengo namba nne lilihusu kutoa elimu bora.
Chapisho hili linalenga kutoa ushauri wa namna ya kuboresha elimu ya msingi katika nchi yetu ya Tanzania.
TAFSIRI YANGU KUHUSU ELIMU YA MSINGI
Elimu ya msingi ni elimu maalumu (formal education) inayomjengea mwanafunzi uwezo wa kusoma, kuandika, kuhesabu na kufahamu mambo ya msingi anayopaswa mtu kuyafahamu na kufahamu angalau kwa kiasi kidogo elimu ya kati (secondary education) ili aweze kufanya vizuri katika elimu ya kati.
BAADHI YA CHANGAMOTO NILIZOZIONA KWA WANAFUNZI WENGI WANAOHITIMU ELIMU YA MSINGI KATIKA NCHI YA TANZANIA
1. Wanafunzi wengi wanaingia kwenye elimu ya kati wakiwa hawajui lugha inayotumiwa kutolea elimu ya masomo mengi ya elimu ya kati (hawajui kingereza).
2. Wanafunzi wengi wanaingia kwenye elimu ya kati wakiwa hawana muelekeo halisi wa masomo ya elimu ya kati, wengi wanaingia kwenye elimu ya kati wakiwa hawajui watamaliza elimu ya kati wakiwa upande upi kimchepuo kwa kuwa wanafunzi huchagua michepuo mwishoni mwa kidato cha pili au mwanzoni mwa kidato cha tatu.
USHAURI WANGU KUHUSU NAMNA YA KUBORESHA ELIMU YA MSINGI KATIKA NCHI YA TANZANIA
1. Wanafunzi wafundishwe na waelewe kuandika, kuongea na kusoma lugha ya Kiswahili na Kingereza.
2. Elimu ya kabla ya kujiunga na elimu ya kati (pre - form one course) itolewe kwa wanafunzi wote waliohitimu darasa la saba katika shule zao za msingi bila malipo au kwa malipo ili kuwapa motisha walimu watakaowapa elimu hiyo.
3. Mwanafunzi anapohitimu elimu ya msingi apewe fursa ya kuchagua mchepuo atakaoutaka ili atakapojiunga na elimu ya kati ajikite katika mchepuo huo, mwanafunzi aamue kama atajikita katika masomo ya sanaa, biashara au sayansi.
4. Elimu ya msingi ijikite katika kufundisha sayansi, uchumi, historia, stadi za kazi, elimu ya mazingira, uzalendo, kusoma, kuandika, kuhesabu, lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa kuwa masomo mengi ya elimu ya kati yanafundishwa kwa lugha la Kingereza.
5. Uwepo mfumo maalumu wa kutambua na kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi.
UMUHIMU WA KUBORESHA ELIMU YA MSINGI KATIKA NCHI YA TANZANIA
1. Elimu ya msingi itamsaidia mtu kuelewa kuhesabu, kuandika na kusoma.
2. Elimu ya msingi itamsaidia mtu kuelewa historia ya taifa lake na historia zingine.
3. Elimu ya msingi itakuza uzalendo.
4. Elimu ya msingi itachangia katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira.
5. Elimu ya msingi itamsaidia mtu kuelewa stadi za kazi.
6. Elimu ya msingi itamsaidia mtu kutambua na kukuza vipaji alivyonavyo.
7. Elimu ya msingi itamsaidia mtu kufanya vizuri katika elimu ya kati kwa kuwa atakuwa na msingi mzuri wa lugha ya Kiswahili na Kingereza.
8. Elimu ya msingi itachangia katika kutatua matatizo yanayoikabili nchi yetu kama vile ukosefu wa ajira, mimba za utotoni nakadhalika.
Faraja Gasto
Mtaalamu wa mipango ya maendeleo,
Simu: +255625775243,
WhatsApp +255767955334.
CC:
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Waziri wa elimu.
3. Wadau wa elimu.
4. Watunga sera.
5. Wadau wa maendeleo ya jamii.
6. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Maoni