NGUVU YA UNAVYOJITAFSIRI


               ✍️Faraja Gasto

Kila mtu kuna namna anavyojitafsiri kutokana na aonavyo nafsini mwake au kutegemeana na picha aliyonayo katika nafsi yake kujihusu yeye mwenyewe.

Hiyo picha unayoiona nafsini mwako kuhusu wewe mwenyewe INA NGUVU YA AJABU SANA KUTEGEMEANA NI PICHA YA AINA GANI.

1. Inaweza kukuvunja moyo.

2. Inaweza kukutia nguvu.

3. Inaweza kukuinua.

4. Inaweza kukushusha.

5. Inaweza kuondoa baadhi ya vitu ndani yako kama vile ujasiri au kujiamini nakadhalika.

SOMA MIFANO HII MICHACHE KUHUSU NGUVU YA UNAVYOJITAFSIRI

1. WAPELELEZI 10

Hesabu 13:33

[33]Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI, NAO NDIVYO WALIVYOTUONA.

Baada ya hawa wapelelezi kuwaona wana wa Anaki, WALIANZA KUJIONA KAMA MAPANZI, yaani picha waliyokuwa nayo nafsini mwao walijiona kama MAPANZI.

Ile picha iliyotokana na walivyojitafsiri ilisababisha

a. Walikata tamaa

b. Wakawakatisha tamaa wengine

c. Wakapoteza ujasiri wa kuendelea na safari

d. Wakaingiwa na roho ya kutokuamini (wakaona Mungu ni muongo)

e. Wakanung'unika nakadhalika

NB: Tatizo lilianza walipojitafsiri kama MAPANZI.

2. DAUDI

Kabla Daudi hajaenda kukabiliana na Goliathi, Daudi alisema "Mimi nimeua Simba na Dubu kwa hiyo hata Goliathi ninaweza kumuua" (1 Samweli 17:34-36)

Ile siku Daudi aliyoua Simba na Dubu alianza KUJIONA KAMA SHUJAA, picha aliyokuwa nayo Daudi nafsini mwake ilimpa nguvu hata kuwa na ujasiri wa kukabiliana na Goliathi, Daudi alikwenda kupigana na Goliathi akiwa na uhakika kuwa atamshinda Goliathi kama alivyowaangamiza Simba na Dubu.

NB: 

1.  Usijitafsiri kutokana na watu wanavyokuona, jitafsiri kulingana na neno la Mungu na kulingana na Mungu anavyokuona.

2. Jenga tabia ya kujifunza neno la Mungu na kuliamini litaondoa picha zisizofaa nafsini mwako.

3. Usiruhusu kujitafsiri tofauti na Mungu anavyokutafsiri.

4. Epuka kuwasikiliza watu wanajitafsiri Vibaya (kama wale wapelelezi Kumi) pia epuka kuwasikiliza watu wanaokutafsiri tofauti na neno la Mungu (wanaoukuambia hauwezi, hautafaulu nakadhalika).

5. Unavyojiona nafsini mwako ndivyo utakavyokuwa pia ndivyo utakavyoishi, hatua ya awali ya kubadili maisha yako ni KUBADILI NAMNA UNAVYOJITAFSIRI. 


Chapisha Maoni

0 Maoni