✍️Faraja Gasto
(Isaya 47:4)
Mungu amekuwa akijitambulisha kwa majina tofautitofauti kwa nyakati tofautitofauti na Kwa watu tofautitofauti, Kuna wakati alijitambulisha kama Niko ambaye Niko, Yahweh, Jehova, Bwana wa majeshi n.k
Mungu alipokuwa akijitambulisha kwa majina tofauti tunaona katika Biblia alitenda kazi kutegemeana na alivyojitambulisha.
Mungu anapojitambulisha kama Bwana wa majeshi kila mtu anatakiwa afahamu kuwa Mungu anamaanisha
a). Anaweza kuokoa
b). Anaweza kumpigania mtu
c). Anaweza kuangamiza
d). Anaweza kuongoza vita
e). Anaweza kufundisha masuala ya vita au mapigano au anaweza kufundisha mbinu za kushinda vita.
f). Anaweza kulinda n.k.
Hivyo basi ukimtegemea Mungu kama Bwana wa Majeshi hakuna vita utakayoshindwa kwa kuwa Bwana wa majeshi atakuwa upande wako kukupa mbinu za kushinda kila aina ya vita.
SOMA MIFANO HII MICHACHE KUHUSU MUNGU ALIVYOFANYA KAZI KAMA BWANA WA MAJESHI
1. Daudi
(Zaburi 144:1)(Zaburi 18:34)
Daudi amepigana vita nyingi alishinda kwa kuwa alikuwa anafundishwa na Mungu mbinu za kushinda vita.
Daudi amewahi kuua Simba na Dubu kwa kutumia mikono yake, mbinu hizo za kukabiliana na Wanyama wakali alifundishwa na Mungu ndio maana wakati anataka kukabiliana na Goliathi hakuogopa umbo la Goliathi Kwa kuwa alijua Mungu ndiye anayemfundisha vita.
2. Mfalme Yehoshafati
(2 Mambo ya nyakati 20:1-30)
Wakati Fulani yaliinuka majeshi yaliyokusudia kumpiga Mfalme Yehoshafati na watu aliowaongoza, Mfalme Yehoshafati na watu wake wakaamua kumuomba Mungu, walipokuwa wakiomba Mungu aliwaambia "vita si yenu ni yangu"
Mungu aliwaambia wasipigane bali wamsifu yeye naye atawapigania.
NB:
1. Mungu ndiye bingwa wa vita, ukimtegemea atakufundisha kupigana vita na hakuna vita utakayoshindwa, Mara nyingi tumeshindwa, tumeshambuliwa kwa kuwa tulizitegemea akili zetu.
2. Katika agano jipya hatufanyi vita Kwa jinsi ya mwili (Kwa kutumia risasi, panga, mqbomu n.k) bali tunafanya vita kwa jinsi ya roho Kwa kuwa tunapigana katika ulimwengu wa roho (2 Wakorintho 10:3-5)(Waefeso 6:10-18)
Mungu anaweza kukufundisha ukawa mshidi katika kila vita.
0 Maoni