MILANGO MIWILI YA UPONYAJI


                  ✍️Faraja Gasto

Sifa mojawapo ya Mungu ni mponyaji, Mungu anaweza kuponya mwili, nafsi, ardhi nakadhalika.

Yamkini umesikia wengine wakisimulia Mungu amewaponya magonjwa ya aina mbalimbali lakini wewe haujapokea uponyaji kutoka Kwa Mungu na unajiuliza kwa nini haujapona, somo hili ni maalumu Kwa ajili yako na kwa ajili ya mtu yeyote anayetaka uponyaji kutoka Kwa Mungu.

Hauwezi kupokea uponyaji wakati umefunga milango, ukifunga milango hauwezi kupokea uponyaji kutoka Kwa Mungu.

Milango ya uponyaji ipo ya aina mbalimbali ila kupitia somo hili utafahamu milango miwili ya uponyaji.

MLANGO WA KWANZA: TOBA

Biblia inafundisha kuwa chanzo kimojawapo cha magonjwa ni dhambi (dhambi ni mlango mmojawapo wa magonjwa, toba ni mlango mmojawapo wa uponyaji) Kwa hiyo Kuna aina za magonjwa huwezi kupona ikiwa haujatubu. Kwa mfano kama umepata UKIMWI kutokana na uzinzi au uasherati ili Mungu akuponye lazima utubu, Mungu akikusamehe mlango wa uponyaji unakuwa wazi.

"Akusamehe maovu yako yote AKUPONYA MAGONJWA YAKO YOTE" (Zaburi 103:3)

"Na kule kuomba kwa imani KUTAMWOKOA MGONJWA YULE, na Bwana atamwinua; HATA IKIWA AMEFANYA DHAMBI, atasamehewa" (Yakobo 5:15)

NB: Kuna uhusiano mkubwa kati ya magonjwa na dhambi.

MLANGO WA PILI: IMANI

Imani ni mlango wa kupitishia mambo mengi kutoka Kwa Mungu kuja Kwa mtu, watu nakadhalika.

Wengine hawapokei uponyaji kwa sababu ya kutokuamini kwao, wengine hawaamini kuwa Mungu anaweza kuponya magonjwa fulani, ni vema ufahamu kuwa MUNGU ANAWEZA KUPONYA UGONJWA WOWOTE ENDAPO UTAAMINI.

"Akamwambia, Binti, IMANI YAKO IMEKUPONYA, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena" (Marko 5:34)

"Yesu akamwambia, Upewe kuona; IMANI YAKO IMEKUPONYA ( Luka 18:42)

NB: Imani ni mlango wa uponyaji, ukiamini utaruhusu uponyaji uingie kwenye mwili wako, nafsi yako nakadhalika.


Chapisha Maoni

0 Maoni