Kama umekuwa unasoma Biblia nina uhakika unafahamu kuwa kuna aina ya maombi huwa yanazaa mambo mbalimbali, baadhi ya mambo yanayozaliwa na maombi hayo ni;-
1. Maombi yanazaa watumishi.
2. Maombi yanazaa miujuza.
3. Maombi yanazaa mazingira fulani.
4. Maombi yanazaa hali fulani.
5. Maombi yanazaa tabia Fulani.
6. Maombi yanazaa mipenyo (breakthroughs).
7. Maombi yanazaa nguvu, ujasiri n.k
NB: Si maombi yote huwa yanazaa, maombi yanayozaa ni maombi ya bidii au maombi ya juhudi YAANI UNAOMBA BILA KUACHA MPAKA UNACHOKIOMBA KITOKEE (PRAYER WITHOUT CEASING), japo unaweza ukaomba mfululizo au ukaomba ombi hilo kila siku n.k
SOMA MIFANO HII
1. MAOMBI YA ELIYA
(Yakobo 5:17-18)
Biblia inasema "Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi ALIOMBA KWA KWA BIDII MAOMBI YAKE YALIZAA MVUA"
Eliya aliomba mvua mara ya kwanza hapakuwa na majibu akaamua kuomba mara saba, mara ya saba kukaonekana dalili ya mvua ndipo akaacha kuomba, soma (1 Wafalme 18:41-45)
2. MAOMBI YA JAMII YA WAAMINIO
(Matendo ya mitume 12:5-11)
Wakati Petro alipotiwa gerezani, Biblia inasema "kanisa likamwomba Mungu Kwa juhudi (prayer without ceasing) yale maombi yalizaa wokovu wa Mtume Petro dhidi ya mikono ya Mfalme Herode aliyetaka kumuua, usiku ule wakati kanisa likiendelea kuomba Malaika alitumwa kumuokoa Mtume Petro.
3. MAOMBI YA BWANA YESU KRISTO
(Marko 14:32-41)
Mwili wa Yesu ulikuwa unamgomea asife msalabani lakini akajikuta ana huzuni iliyomfanya kukosa amani, akaenda kuomba kwamba "saa hiyo au kikombe Kile kimuepuke lakini si kama nitakavyo Mimi bali kama utakavyo Mungu Baba"
Alipoomba mara ya kwanza hakukuwa na matokeo tofauti aliyoyaona, akaomba mara pili hakukuwa na matokeo tofauti aliyoyaona, akaomba mara ya tatu ndipo akaona matokeo tofauti baada ya hapo ndipo akaacha kuombea agenda ile iliyompeleka Gethsemane.
Maombi ya Yesu yalizaa ujasiri wa kuukabili msalaba na kutembea kwenye mapenzi ya Mungu Baba.
0 Maoni