(Mathayo 9:38)
Yesu alipokuwa duniani alifundisha aina mbalimbali za maombi, aina mojawapo ya maombi ambayo Yesu alifundisha ni MAOMBI YANAYOZAA WATENDAZI (Watumishi).
"Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Pray ye therefore the Lord of the harvest, that he will send forth labourers into his harvest" (Mathayo 9:38)
Maombi yanayozaa watenda kazi ni ya aina gani?
JIBU: Ni maombi yenye ujumbe usemao "Mungu peleka watenda kazi katika eneo Fulani au Mungu inua watenda Kazi katika eneo Fulani"
Hii ni aina ya maombi ambayo si watu wengi wanaomba, aina hii ya maombi ni ya muhimu sana kama zilivyo aina zingine za maombi ndio maana Bwana Yesu alisema "BASI MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDAKAZI"
Bwana Yesu alitaka tujue kuwa watenda Kazi huwa wanapelekwa kazini sio tu Kwa kuwa Mungu ametaka kuwapeleka bali kwa kuwa kuna mtu au watu wameomba Mungu kwa ajili ya jambo fulani.
Maombi haya yanaweza kuzaa watendakazi au watumishi wa Mungu Katika kanisa, katika taifa na Katika Dunia.
NB: JIZOEZE KUOMBA MAOMBI HAYA ILI MUNGU AINUE WATENDAKAZI KATIKA MAENEO MBALIMBALI.
0 Maoni