✍️Faraja Gasto
UTANGULIZI
Suala la kunena kwa lugha halijafundishwa kwa kina makanisani ndio maana limeonekana halina umuhimu, madhehebu mengine yanapinga suala la kunena kwa lugha japo yanakubali Roho Mtakatifu yupo na anatenda kazi, kukosekana kwa mafundisho ya kina kumepelekea wengine kupotosha suala la kunena kwa lugha.
Chapisho hili linalenga kuwapa watu mwanga kuhusu kunena kwa lugha.
KUNENA KWA LUGHA NI NINI?
1. Ni kuongea lugha zilizopo duniani au lugha ambazo hazipo duniani kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.
2. Ni kuongea lugha ambayo haujajifunza au lugha isiyo yako kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.
HISTORIA YA KUNENA KWA LUGHA
Adamu ndiye mtu wa kwanza kunena kwa lugha, Adamu hakuzaliwa ila aliumbwa akapewa lugha ya kutumia, lugha ile iliwekwa ndani yake na Roho Mtakatifu (Mwanzo 2:15-17)
Pia watu waliokuwa wanajenga mnara wa Babeli walinena kwa lugha mbalimbali kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, zile lugha walipewa na Roho Mtakatifu (Mwanzo 11:7-9)
Nijibu maswali yafuatayo,
1. Je! mtu asiponena kwa lugha ni ishara kuwa Roho Mtakatifu hayumo ndani yake?
2. Je! mtu asiponena kwa lugha haendi mbinguni?
3. Je! Biblia inasema nini kuhusu kunena kwa lugha?
JIBU LA SWALI LA 1
Kutokunena kwa lugha sio ishara ya kutokuwa na Roho Mtakatifu ndani ya mtu, Roho Mtakatifu huingia ndani ya mtu pale mtu anapomwamini Yesu kwa hiyo kila aliyemwamini Yesu ana Roho Mtakatifu ndani yake haijalishi ananena au haneni kwa ndimi (1 Wakorintho 12:30)
JIBU LA SWALI LA 2
Kunena kwa lugha sio tiketi ya kuingia mbinguni, tiketi ya kuingia mbinguni ni moyo safi unaotokana na utakatifu (Mathayo 5:8)(Waebrania 12:14)
JIBU LA SWALI LA 3
1. Kunena kwa lugha ni ishara mojawapo ya kumwamini Yesu (Marko 16:17)
2. Ni ishara mojawapo ya kujazwa au kushukiwa na Roho Mtakatifu (Matendo ya mitume 2:4, 10:44-46)(Mwanzo 11:7-9)
3. Ni ishara mojawapo ya utendaji kazi wa karama ya aina za lugha (1 Wakorintho 12:10d)
Je! kwa nini wengine hawaneni kwa lugha?
Ziko sababu nyingi ila baadhi ya sababu ni
1. KUTOFAHAMU KWELI ISEMAVYO KUHUSU KUNENA KWA LUGHA
Mtu asiyefahamu kweli kuhusu kunena kwa lugha hawezi kuwa huru kunena kwa lugha pia hawezi kupokea uwezesho wa kunena kwa lugha (Yohana 8:32)
2. KUMZIMISHA ROHO MTAKATIFU (1 Wathesalonike 5:19)
Kumzimisha Roho wa Mungu ni kumkatalia Roho Mtakatifu asitende kazi au asidhihirike kutoka ndani yako.
3. HOFU
Watanionaje?
Watanitafasirije?
Hofu ni kizuizi kikubwa cha kupokea mambo ya Roho Mtakatifu (2 Timotheo 1:6-7)
4. KUTOKUONGEA LUGHA AMBAYO ROHO MTAKATIFU ANAILETA KWENYE UFAHAMU AU KWENYE ULIMI
(Matendo ya mitume 2:4)
Biblia inasema wakajazwa Roho Mtakatifu "WAKAANZA KUSEMA KWA LUGHA NYINGINE" Roho anapoleta lugha ndani yako ANZA KUSEMA KWA LUGHA HIYO.
Barikiwa kwa elimu hiyo ya awali.
0 Maoni