✍️ Faraja Gasto
(Matendo ya mitume 3:19)
Chanzo kikuu cha matatizo yote ni DHAMBI.
Tatizo mojawapo linalosababishwa na dhambi ni kupoteza furaha, kukosa furaha au kuwakosesha wengine furaha.
Dhambi ni mlango unaopitisha matatizo mengi sana ikiwemo kuondoa furaha.
(Zaburi 51:4,12)
Mfalme Daudi aligundua kuwa dhambi iliondoa furaha katika maisha yake ndio maana alitubu na akamwambia Mungu "UNIRUDISHIE FURAHA YA WOKOVU WAKO"
(Luka 15:14-16)
Huyu kijana alijikuta amepoteza furaha kwa sababu ya dhambi lakini alipotubu furaha ilirejea tena (Luka 15:17-24)
Je! umepoteza furaha?
Biblia imeweka wazi kuwa kutubu kunaweza kubadilisha NYAKATI, wakati wa furaha au wa kuburudishwa unaweza kuja endapo mtu au watu watatubu (Matendo ya mitume 3:19)
Barikiwa.
0 Maoni