MAMBO YA KUFANYA ILI IBILISI ASIKUONEE

 


                       ✍️Faraja Gasto

Biblia imetuambia waziwazi kuwa Ibilisi anaweza kuonea watu kwa namna mbalimbali

Matendo ya Mitume 10:38

"Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye"

Sasa ukitaka Ibilisi asikuonee kuna mambo ya kufanya, baadhi ya mambo ni

1. IFAHAMU KWELI (WEKA NENO LA MUNGU KWA WINGI MOYONI MWAKO)

"tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru" Yohana 8:32

Kadiri unavyoifahamu kweli ndivyo unavyopunguza kiwango cha kuonewa na Ibilisi.

2. TAKA SANA KUJAA ROHO MTAKATIFU KILA WAKATI PIA YATAKE MAFUTA YA ROHO MTAKATIFU (annointing)

Kazi mojawapo ya mafuta ya Roho Mtakatifu ni kukupa uwezo wa kushughulikia uonevu wa Ibilisi katika maisha yako na maisha ya watu wengine.

"habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye" (Matendo ya mitume 10:38)

3. UWE MDAU WA MAOMBI 

Yaani kuomba iwe tabia yako, uwe mwombaji Kwa kuwa shetani anaonea sana watu wasioomba pia watu wasio na maarifa.

(Waefeso 6:10-12)


4. EPUKA KUABUDU MIUNGU MINGINE (Waamuzi 10:6,8)

Wana wa Israeli walipoabudu mingine walifungua mlango wa kuonewa na kusumbuliwa.


5. MWAMINI BWANA YESU AWE BWANA KATIKA MAISHA YAKO (Matendo ya mitume 10:38)

Yesu ndiye mwenye uwezo wa kukuokoa dhidi ya uonevu wa Ibilisi.


Chapisha Maoni

0 Maoni