KUKUMBUKA AHADI ZA MUNGU NA KUAMINI MUNGU ATAFANYA KAMA ALIVYOAHIDI

 


                   ✍️ Faraja Gasto

Yapo mambo mengi Mungu aliyaahidi Kwa ajili ya wana wa Israeli, jambo mojawapo ni kuwatoa katika nchi ya Misri na kuwapeleka Kanaani.

Ulifika wakati sahihi Mungu akawatoa kwenye utumwa lakini Katika safari ya kuelekea Kanaani walikumbana na matatizo njiani (kupita mahali hakuna maji, hakuna vyakula walivyotaka n.k) wana wa Israel walijikuta wamesahau ahadi ya Mungu kwao hatimaye hawakumwamini Mungu, kutokana na kutokuamini Kwao walimnung'unikia Mungu hatimaye wengi waliishia njiani hawakufika Kanaani.

NB: Hata sasa watu wengi wanapokumbana na matatizo mbalimbali wanajikuta wamesahau ahadi za Mungu kwa ajili yao na hatimaye wanaanza kuona kama Mungu hawajali, Mungu amewasahau nakadhalika.

Nataka nikuambie kuwa Mungu hajawahi kusahau alichoahidi hivyo basi kukabiliwa na matatizo sio kipimo kwamba Mungu amekusahau au Mungu hakujali.

Mungu ndiye aliyewaongoza wana wa Israel kupita kwenye njia ambayo hapakuwa na maji lakini akawatolea maji kwenye mwamba, Mungu ndiye aliyewaongoza wana wa Israeli kupita kwenye njia ambayo walikutana na Bahari ya Shamu lakini Mungu aliwavusha.

Ni muhimu sana ukumbuke kuwa Mungu ni mwaminifu sana katika kutimiza ahadi zake hivyo basi hata kama unaona mbele kuna giza, hakuna wa kukusaidia, umefika mahali umejeruhiwa nakadhalika HEBU IKUMBUKE AHADI YA MUNGU KWAKO, AMINI MUNGU ATATIMIZA AHADI ZAKE KWAKO, SONGA MBELE Kwa kuwa matatizo hayawezi kumzuia Mungu kutimiza ahadi zake.

(Hesabu 23:19)

Barikiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni