WAZO LA MUNGU LINAVYOKUJA KAMA SWALI


                       Faraja Gasto

Mungu anayo mawazo yake (Yeremia 29:11)(Isaya 55:8)


Mawazo ya Mungu huja kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya swali yaani wazo la Mungu linaweza kukufanya ujikute unajiuliza swali au maswali japo si wengi huwa wanapambanua kwamba wazo la Mungu limekuja mioyoni mwao.


(2 Wafalme 7:3)
Hawa wakoma walijikuta wamepata wazo la Mungu likaja kama swali wakajikuta wanajiuliza "mbona tunakaa hapa hata tufe?" walipotendea kazi wazo lile Mungu alitembea nao.


(Luka 15:17)
Huyu kijana alipokuwa katika hali ngumu ya kiuchumi alipata wazo la Mungu, wazo lilikuja kama swali akajikuta anajiuliza "ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza na mimi hapa ninakufa kwa njaa". Huyu kijana alipotendea kazi lile wazo la Mungu hali yake ya kiuchumi ilibadilika.

Ni mara ngapi Mungu amekuwa akikupa wazo lake na ukajikuta unajiuliza maswali fulani?


NB: Jifunze kutendea kazi wazo la Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni