BAADHI YA AINA ZA AKILI ZA MUNGU

 

                     Faraja Gasto

Mungu ana akili za aina nyingi ndio maana Biblia inasema "akili zake hazichunguziki" (Isaya 40:28)


Zifuatazo ni baadhi ya aina za akili za Mungu;-

1. AKILI ZA VITA

(1 Samweli 18:5)

Mungu alimpa Daudi akili za vita ndio maana Daudi aliwahi kuua simba na Dubu, aliua Goliathi hatimaye akaingizwa kwenye jeshi la Mfalme Sauli.


Akili za vita zilimfanya Daudi akawekwa juu ya watu wa vita, alikuwa anapewa akili za vita na Mungu (Zaburi 18:34,37,38)


Kumbuka Mungu anaitwa BWANA WA MAJESHI kwa hiyo anazo akili za vita.


2. AKILI ZA KUMTUMIKIA MUNGU AU AKILI ZA UTUMISHI

(Kutoka 35:30-35)

Akili za utumishi zinampa mtu kuelewa namna ya kufanya kazi za Mungu.


3. AKILI ZA KUJUA NYAKATI 

(1 Mambo ya nyakati 12:32)

Mungu aliwapa wana wa Isakari akili za kujua nyakati wawe msaada kwa waisraeli wenzao.


Akili hizi zinampa mtu kuelewa cha kufanya katika kila nyakati (Mhubiri 3:1)


4. AKILI ZA KUPANGA MIPANGO NA KUIFANIKISHA.

Yusufu alipewa na Mungu akili hizi (Mwanzo 41:33,39)

Chapisha Maoni

0 Maoni