UMUHIMU WA KUMPA MUNGU NAFASI YA KUTATUA MATATIZO YALIYOPO KATIKA NCHI ZETU


Mungu ndiye bingwa wa kutatua matatizo ndio maana hakuna linalomshinda (Mwanzo 18:14a)


Yapo matatizo ambayo yameendelea kuwepo katika nchi zetu (rushwa, ufisadi, ukeketaji, ukandamizaji wa haki, dhuluma nakadhalika) kwa kuwa 

1. Watu wamemkataa Mungu, hawajampa Mungu nafasi ya kutatua matatizo hayo.


2. Wanasiasa wanaaminiwa kuliko Mungu.


3. Tunategemea wataalamu badala ya kumtegemea mtaalamu wa wataalamu (Mungu)


NCHI YA MISRI iliwahi kuepuka tatizo la njaa lililowahi kuikumba dunia kwa kuwa Misri ilimpa Mungu nafasi ya kuwasaidia (Mwanzo 41:34-43)


TUNAWEZAJE KUMPA MUNGU NAFASI YA KUTATUA MATATIZO YA NCHI ZETU?

1. Kufuata maelekezo ya Mungu yaliyomo ndani ya Biblia.


2. Kufuata maelekezo ambayo Mungu anayatoa kupitia vinywa vya watumishi wake.


3. Kuwaendea watumishi wa Mungu ili kumsikia Mungu anasemaje kuhusu matatizo yaliyopo kwenye nchi zetu.

Chapisha Maoni

0 Maoni