JE! NI SAHIHI MTUMISHI WA MUNGU KUWA NA WALINZI


                     Faraja Gasto

Chapisho hili ni mtazamo au hoja yangu binafsi kuhusu watumishi kuwa na walinzi.

Nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu ulinzi na usalama kama ifuatavyo;-

1. Hakuna anayeweza kuwa salama bila ulinzi kwa kuwa USALAMA NI MATOKEO YA ULINZI.


2. Kila mwanadamu ana walinzi katika mwili wake waitwao KINGA ZA MWILI.


3. Kuvaa viatu, kulala ndani ya chandarua, kufunga milango, kuweka vitasa, makufuri na makomeo, kuweka fedha benki, kuvaa nguo nakadhalika NI KUJIWEKEA ULINZI KWA KUWA VIATU, NGUO, CHANDARUA NAKADHALIKA NI WALINZI.


4. Wazazi na walezi wa kimwili au wa kiimani NI WALINZI.


MTAZAMO WANGU

Suala la watumishi kuwa na walinzi haliwezi kutafsiriwa moja kwa moja kama kutomwamini Mungu lakini kama mtu ana walinzi HATAKIWI KUHUKUMIWA PIA HATAKIWI KUWEKA TUMAINI NA KUWATEGEMEA WANADAMU BALI ANATAKIWA KUMTEGEMEA MUNGU TU.


NB: Ni kweli Mungu anaweza kuwalinda watumishi wake dhidi ya kila silaha (Isaya 54:17) LAKINI MUNGU HAJAMZUIA MTU KUCHUKUA TAHADHARI.

Chapisha Maoni

0 Maoni