Faraja Gasto
1. Kaa mbali na watu hao yaani kaa nao mbali kijografia.
(Mathayo 2:13-14)
- Yusufu na mkewe walihamia Misri kwa muda ili kumnusuru Yesu asiuawe.
(Mwanzo 27:42-45)
Yakobo alikimbilia ujombani ili kuepuka kuuawa.
(1 Samweli 20:42, 22:1)
Daudi alimkimbia Mfalme Sauli ili asiuawe.
2. Usimuamini mtu yeyote kupita kiasi, ni vema uchukue tahadhari.
(1 Samweli 3:22-30)
Jemedari Abneri aliuawa kutokana na ulaghai akaingizwa kwenye mtego wa mauti.
3. Jizoeze kubadili njia za kupita na mitindo ya kuingia na kutoka mahali fulani (nyumbani kwako, kazini n.k)
(Yoshua 2:22)
Wapelelezi waliingia Yeriko kwa njia nyingine pia walitoka kwa njia nyingine.
(Mathayo 2:12)
Mamajusi waliingia Bethlehemu kwa njia nyingine pia walitoka kwa njia nyingine.
Kumbuka wanadamu tunaingia duniani kwa njia ya kuzaliwa ila tunaondoka kwa njia ya kufa.
NB: Ni kweli Mungu anaweza kukulinda dhidi ya maadui ila usipuuze mbinu hizo tatu kwa kuwa ni mbinu za kibiblia.
0 Maoni