Zipo kanuni mbalimbali za ufundishaji kwa mujibu Biblia.
Kanuni mojawapo ni FUNDISHA KILE UNACHOTENDA.
-->Hautakiwi kufundisha usiyoyatenda, fundisha unayoyatenda, usiwafundishe watu unyenyekevu ikiwa wewe umejaa kiburi.
(Matendo ya mitume 1:1)
Yesu alifundisha aliyokuwa akiyafanya (alifundisha aliyoyaishi)
(Ezra 7:10)
Ezra alifundisha aliyoyafanya yaani aliyoyaishi ndiyo aliyoyafundisha.
(1 Wakorintho 11:1-2)
Mtume Paulo alikuwa na ujasiri wa kuwaambia wakorintho wajifunze kwake kwa kuwa aliyaishi aliyokuwa akiyafundisha.
(1 Timotheo 4:11-16)
Mtume Paulo alimfundisha Timotheo ayatendee kazi anayoyafundisha.
Kutendea kazi unayoyafundisha ni kanuni mojawapo ya ufundishaji.
0 Maoni