FAIDA ZA KUTEGEMEA AKILI ZA MUNGU


                    Faraja Gasto

Mungu hajazuia mtu kutumia akili ila Mungu hataki tuzitegemee akili zetu (Mithali 3:5-6)


Faida za kutegemea akili za Mungu

1. Akili za Mungu zitakusaidia kutenda tofauti na wengine.

(Mwanzo 41:33,39,53-57)

Yusufu alikuwa na akili za Mungu akaisaidia nchi ya Misri kutenda tofauti na nchi zingine, wakati mataifa mengine yanakula chakula bila kuweka akiba, taifa la Misri lilikuwa linaweka akiba hatimaye likanusurika na njaa ya miaka 7.


2. Akili za Mungu zitakupa mtazamo tofauti na wengine.

(1 Samweli 17:34-37)

Wakati wengine wanamuona Goliathi kama tishio, Daudi alimuona Goliathi sio tishio.


Daudi alimkabili  Goliathi kwa akili za Mungu, Daudi hakumkaribia Goliathi alimshambulia Goliathi akiwa mbali, Daudi alipewa na Mungu hiyo akili.


3. Akili za Mungu zitakusaidia kupanga na kutekeleza mikakati ya kufanikisha mipango.

(Mwanzo 41:33,39)

Yusufu alikuwa na akili za Mungu, akili hizo zilileta mpango wa kulinusu taifa la Misri na njaa na mikakati ya kufanikisha mpango huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni