Faraja Gasto
Huu
ni utumishi ambao unamfanya mtu aamue kwa hiari yake au kwa gharama zake
kufanya jambo fulani jema bila kuombwa au kulazimishwa.
Mtu
anaweza kuamua
*kujenga
shule au chuo peke yake.
*kumnunulia
gari au kumjengea nyumba mchungaji.
*kufagia
kanisa, kupamba kanisa, kununua vyombo vya muziki n.k
*kufundisha
watoto au vijana kuhusu mambo mbalimbali.
*kujenga
kanisa, kulipia gharama za mikutano ya injili.
*kutunza
wajane na yatima.
*kugawa
biblia mashuleni, vyuoni n.k
*Kuombea
nchi, watumishi n.k.
*kuwatetea
wanaoonewa.
*kutumia
elimu kuisaidia jamii.
*kuisaidia
serikali kutatua matatizo katika nchi.
(1
MAMBO YA NYAKATI 22:1-11)
Mfalme
Daudi alijitolea kujenga hekalu peke yake, akaanza kuweka akiba kwa ajili ya
ujenzi.
(MATENDO
YA MITUME 9:36-40)
Dorkasi
alijitolea kuwavalisha wajane.
(LUKA
7:1-10)
Huyo
akida alijitoa kwa taifa akajenga sinagogi kwa gharama zake.
HITIMISHO
Je!
wewe unajitolea kufanya nini?
0 Maoni