MBINU KADHAA ZA KUSHINDA MAWAZO MABAYA


 Faraja Gasto

Utangulizi

Mawazo mabaya ni mawazo yoyote ambayo yako kinyume na neno la Mungu au mpango wa Mungu.

Watu wengi wanasumbuliwa na mawazo mabaya, mawazo mabaya ndio yanayowafanya watu kufanya maamuzi mabaya, somo hili ni mahsusi kwa kila anayesumbuliwa na mawazo mabaya.

 

MBINU KADHAA ZA KUSHINDA MAWAZO MABAYA

1.      Weka neno la Mungu moyoni mwako [Zaburi 119:11]

 

2. Tumia maombi kuangusha mawazo mabaya

[2 Wakorintho 10:5]

 

3. Jifunze kusamehe waliokukosea [Mathayo 6:12]

Kila ambaye hajasamehe waliomkosea huwa anasumbuliwa na mawazo mabaya.

 

4. Jifunze kuridhika [Wafilipi 4:11-12]

Ridhika na kipato chako, mke, mume n.k

 

5. Msikilize Mungu

[Mathayo 1:18-25]

Yusufu alitaka kumuacha Mariamu kwa kuwa aliona ana mimba kabla hawajakutana kimwili lakini Mungu aliingilia kati kuharibu hayo mawazo mabaya ya Yusufu.

 

6. Ruhusu upendo ukutawale [1 Wakorintho 13:4-7]

Barikiwa pia washirikishe wengine somo hili.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni