Faraja Gasto
Kuna
jambo nataka nikufundishe wewe ambaye umekuwa na malengo halafu hayakutimia.
(Luka
19:1-5)
Ukisoma
andiko hilo utakutana na kisa cha mtu aliyeitwa Zakayo aliyekuwa na lengo la
kutaka kumwona Yesu ni mtu wa namna gani.
Vikwazo
vilivyosababisha asimwone Yesu
1.
Umati wa watu
2.
Ufupi wa kimo (alikuwa mfupi)
ZAKAYO
HAKUBADILI LENGO BALI ALIBADILI MBINU, aliamua kupanda juu ya mti uitwao mkuyu,
Yesu alipopita pale akamwona zakayo yuko juu ya mti, Yesu akamwambia ashuke
upesi maana atakwenda kushinda mchana kutwa kwa zakayo.
NAMI
NAKUFUNDISHA usiyatupitie mbali malengo ambayo hayajatimia, tathmini vikwazo
vilivyosababisha malengo yasitimie kisha badili mbinu (buni mikakati mipya
itakayosababisha malengo yatimie).
0 Maoni