Faraja Gasto
Mungu huongea nasi mambo mbalimbali
kwa njia mbalimbali kama ndoto, maono, kwa kusoma neno, kwa kusikiliza mahubiri
au mafundisho, kwa kusoma vitabu, kushuhudia katika dhamiri na roho zetu n.k,
wakati mwingine tunajikuta tunasahau, kwa mfano kuna wakati Mungu anampa mtu
wimbo, taarifa, maelekezo au mafundisho kwa njia ya ndoto halafu ghafla mtu
anasahau, kunena kwa lugha kunaweza kukusaidia kukumbuka.
(Yohana 14:26)
"lakini huzo Msaidizi, huyo Roho
Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na
KUWAKUMBUSHA YOTE NILIYOWAAMBIA"
Roho Mtakatifu ana kazi ya
kukukumbusha mambo ambayo Mungu aliyokuambia.
Ndoto ngapi huwa unazisahau? kama
zipo basi ujue kuwa kama zina ujumbe wa Mungu na umezisahau, njia mojawapo ya
kuzikumbuka ni kuomba kwa kunena kwa lugha.
Kama kuna mambo Mungu alikuambia kwa
njia yoyote ukasahau, unapoomba kwa kunena kwa lugha, Roho Mtakatifu
atakukumbusha.
0 Maoni