ROHO MTAKATIFU ANAVYOWEZA KUTUFANYA KUWA NURU YA ULIMWENGU


 Faraja Gasto

Kufuatana na Mathayo 5:14-16 kila aliyemwamini Yesu anaitwa NURU YA ULIMWENGU.

Iko hivi, kuwa nuru ni kitu kingine na kuangaza ni kitu kingine, pia ili nuru iangaze lazima taa iwake, lazima kuwepo na nguvu au chanzo kinachosababisha taa kuwaka yamkini chanzo ikawa maji, mafuta, jua, upepo n.k

Kwa mantiki hiyo ni kwamba kama waliomwamini Yesu wanaitwa NURU YA ULIMWENGU lazima ipo nguvu au chanzo kinachosababisha mwangaza kutokea kwenye hiyo nuru.

Chanzo au nguvu inayowafanya watu waliomwamini Yesu wafanyike nuru ya ulimwengu ni ROHO MTAKATIFU.

Ndio maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa wasitoke Yerusalemu mpaka ROHO MTAKATIFU atakapowajilia (Matendo ya mitume 1:4,5,8)

Wanafunzi wa Yesu walipojazwa Roho Mtakatifu ndipo wakaanza kuangaza; wakahubiri, wakaponya, wakafufua n.k

NB: Hauwezi kuangaza bila Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu ndiye chanzo au nguvu inayosabisha nuru yetu iangaze.

Tumtake sana Roho Mtakatifu ili tukaangaze.

Tukiangaza watu wataona matendo yetu mema kisha watamtukuza Mungu.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni