Faraja Gasto
TABIA
YA 1: Huwa wanakimbia baada ya kufanya uhalifu.
(Kutoka
2:13-15)
TABIA
YA 2: Huwa wanajificha wakati wa kufanya au baada ya kufanya uhalifu.
(Mwanzo
3:7-10)
-Katika
harakati za kujificha huwa wanajipa majina bandia, huwa wanafunika nyuso zao,
huwa wanabadili mazingira n.k
TABIA
YA 3: Huwa wana tabia ya kuharibu au kupoteza ushahidi.
(Kutoka
2:11-12)
TABIA
YA 4: Macho ya mhalifu huwa hayatulii, huwa yanatazama huku na kule ili
ajiridhishe hakuna anayemuona au kumshtukia.
(Kutoka
2:12)
TABIA
YA 5: Mara nyingi wahalifu huwa wana wasiwasi au mashaka, hawajiamini.
(Matendo
ya mitume 5:1-5)
-Wasiwasi
au mashaka aliyokuwanayo Anania yalimfanya Petro afahamu kuwa Anania amefanya
uhalifu.
TABIA
YA 6: Wahalifu huwa wana tabia ya KUKATAA AU KUKWEPA
UKAGUZI AU UPEKUZI (MWANZO 31:34-35).
Zipo
sababu nyingi zinazopelekea watu kukataa kukaguliwa au kupekuliwa, sababu
mojawapo ni UHALIFU, kama mtu amebeba magendo au bidhaa haramu au ana silaha
haramu lazima atakwepa au atakataa kukaguliwa au kupekuliwa.
0 Maoni