MABORESHO
NI NINI?
a). Kutengeneza
muonekano mpya wa kitu, mtu au watu, eneo, jengo n.k.
b). Kukiongezea
kitu uwezo wa kufanya jambo fulani au kumuongezea mtu uwezo wa kufanya jambo
fulani.
c). Kukiongezea
kitu thamani au kumuongezea mtu thamani.
d). Kutengeneza
ladha mpya.
e). Kuanzisha
mfumo, mbinu au utaratibu mpya.
ISHARA
ZINAZOONYESHA KUHITAJIKA KWA MABORESHO
1.
Kujirudia kwa tatizo fulani katika familia, jamii, mkoa, nchi n.k.
2.
Kulemewa na mzigo fulani (majukumu n.k)
3.
Mabadiliko ya nyakati, misimu, mazingira, utawala na kizazi.
4.
Kuongezeka kwa watu, mifugo, watoto, wateja, majukumu na kipato.
5.
Kupata hasara.
6.
Kutotimiza malengo.
7.
Watu kutotimiza wajibu wao.
8.
Kuzorota au kudorora kwa uchumi, taasisi, kampuni n.k
9.
Kipato kutokukidhi mahitaji, makazi kutokukidhi mahitaji kutegemeana na idadi
ya watu.
10.
Ugumu wa kupata huduma fulani, kufika mahali fulani n.k
MBINU
ZA KUFANYA MABORESHO
1.
Kugawa majukumu kwa wengine (delegation)
2.
Kufanya vikao.
3.
Kuongeza idadi ya wafanyakazi, vitendea kazi, vyanzo vya mapato, vituo vya
kutolea huduma n.k.
4.
Kuwapeleka watu masomoni au kuwapatia watu elimu.
5.
Kubadili mfumo au mtindo.
6.
Kuwa na vipaumbele.
7.
Kuongeza muda wa kufanya jambo fulani.
8.
Kuongeza ukubwa wa chombo, nyumba, barabara, daraja n.k
NINI
CHA KUBORESHA?
1.
Watu
-Kuwapatia
elimu, wajibu, mamlaka n.k
2.
Miundombinu
-Kuongeza
miundombinu, kupanua miundombinu n.k
3.
Kazi
-Kuongeza
wafanyakazi, vitendea kazi, vituo vya kutolea huduma n.k
4.
Mfumo
-Kutunga
sheria mpya, kuanzisha utaratibu mpya n.k
KANUNI
ZA KUFANYA MABORESHO
1.
Kiwepo cha kuboresha.
2.
Ushirikishwaji wa watu au wadau.
3.
Kuwa tayari kulipa gharama kwa ajili ya maboresho.
4. Kufanya
tathmini na kuainisha matatizo.
5.
Kuweka malengo.
6.
Kuweka vipaumbele.
7.
Kuandaa mikakati na kuitekeleza.
0 Maoni