Faraja Gasto
Hii
ni roho chafu inayowafanya watu kusahaulika pia inayafanya maeneo kusahaulika.
Ndio
maana unakuta watu wamechumbiana halafu mmoja akaenda kusoma lakini akamsahau
mchumba wake akapata mchumba mpya.
Ndio
maana unakuta mtu anamuaga mkewe kuwa anakwenda kutafuta pesa mahali fulani
lakini akizipata anamsahau mkewe, anasahau kama ameacha familia kisha anaoa
tena.
Ndio
maana unakuta mtu anawatendea watu mema lakini wakifanikiwa wanamsahau.
Ndio
maana unakuta mtu anajitoa kusomesha watoto wake lakini watoto wakifanikiwa
wanamsahau.
Hii
roho ikikaa juu ya eneo, eneo hilo halitapata maendeleo hata kwenye mipango ya
maendeleo halitajadiliwa.
(Esta
2:21-23)
roho
ya kusahaulika ilisababisha Mordekai hakukumbukwa, japo alitenda jambo jema
lakini hakukumbukwa.
Maombi
ya kufunga siku tatu yalishughulikia mambo mbalimbali katika ulimwengu wa roho,
maombi yale yalishughulikia roho ya kusahaulika.
Ona kilichotokea baada ya yale maombi, MORDEKAI ALIKUMBUKWA na akatendewa mema, soma (Esta 6:1-11)
(Mwanzo
40:14-15)
Baada
ya Yusufu kuwatafsiria watu wawili ndoto, Yusufu alimwambia mmoja kuwa
"utakapopata mema UNIKUMBUKE"
Lakini
pamoja na kumwambia amkumbuke, yule mtu hakumkumbuka Yusufu.
Roho
ya kusahaulika ndio ilisababisha Yusufu asahaulike.
NB:
Japo Yusufu alikuwa gerezani lakini ALIKUWA ANAMUOMBA MUNGU AMTOE HUMO, kama
alimwambia mfungwa mwenzake akitoka amkumbuke (Mwanzo 40:14) basi uwe na
uhakika alikuwa anamuomba Mungu amtoe gerezani.
Sasa ona kilichotokea baada ya miaka miwili, Mfalme Farao akaota ndoto halafu akakosekana mv wa kutafsiri ndoto (Mwanzo 41:1-8)
Yule
mtu ambaye alitafsiriwa ndoto na Yusufu ndipo alipomkumbuka Yusufu, ona
alichosema "nayakumbuka makosa yangu leo (Mwanzo 41:9)
Baada ya hapo akamjulisha Mfalme Farao kuwa yupo mtu anayeweza kutafsiri ndoto yako (Mwanzo 41:9-13)
Ndipo
Farao akaagiza Yusufu atolewe gerezani (Mwanzo 41:14-45)
NB:
roho ya kusahaulika inaweza kumfanya mtu asahaulike, shughulikia roho hii kwa
njia ya maombi.
0 Maoni