Faraja GastoSiku
moja niliona maono haya, nilikuwa napita mahali fulani palikuwa na ghorofa,
kule ghorofani palikuwa na mtu anawanyunyizia maji watu wanaopita jirani na ile
ghorofa.
Nami
nilipopita nikanyunyiziwa maji kisha nikaenda mbele nikiwa natafakari,
nilipofika mbele kidogo nikaona kijana anawamwagia watu maua nami nilipopita
akanimwagia maua nikaondoka huku natafakari maana ya mambo hayo.
Nilipoendelea
mbele nikaona kijana fulani anawaelekeza watu pa kupita, nilipofika mimi
nikakataa kwenda kule alikoelekeza ghafla akajaa ghadhabu nilipoona amebadilika
nikakemea kwa jina la Yesu akaanguka chini.
Nilipoendelea
mbele kidogo akatokea binti ameghadhibika nikakemea kwa jina la Yesu akaanguka,
ghafla akatokea binti mwingine akajilaza kwenye mwili wa yule aliyeanguka kisha
akainuka akaninyooshea kidole, katika kidole chake kukatoka vitu kama kalamu
zinanijia kwa kasi ghafla nikasikia sauti ikiniambia "sema nazuia kwa damu
ya Yesu" niliposema maneno hayo nikashtuka toka kwenye maono hayo.
CHA KUJIFUNZA: Kuna wakati ukilitumia jina la Yesu hauoni matokeo ila ukitumia damu ya Yesu utaona matokeo, ila ni muhimu Roho Mtakatifu akuongoze katika kutumia jina la Yesu na damu ya Yesu.
0 Maoni