Faraja Gasto
Wapo
watu wengi wana tatizo la kutumia fedha vibaya, matumizi mabaya ni pamoja na
kununua vitu ambavyo haukupanga kuvinunua.
Mbinu za kukusaidia kuepuka manunuzi ambayo
haukuyapanga
1.
ANDIKA KILA UNACHOTAKA KUNUNUA SIKU HIYO
-Usiende
dukani, mnadani au sokoni bila orodha ya vitu unavyotaka kununua.
2.
EPUKA KUPITA MAHALI AMBAPO BIDHAA ZINAUZWA
-Ukipita
mahali ambapo bidhaa zinauzwa ni rahisi kujikuta umenunua kitu ambacho
haukupanga kununua.
3.
EPUKA KUMSIKILIZA MUUZA BIDHAA
-Ikiwa
hauna mpango wa kununua bidhaa usimsikilize muuza bidhaa kwa kuwa katika
kusikiliza utajikuta umeshawishika kununua kitu ambacho haukupanga kununua.
4.
EPUKA KUTEMBEA NA FEDHA KATIKA MFUKO
-
Fedha huwa inamshawishi na kumtengenezea mtu kiu au njaa itakayompelekea
kununua kitu ambacho hakupanga kununua. Tembea nayo katika mfumo wa
kielektroniki (M-pesa, Tigopesa n.k)
5.
EPUKA KUULIZA BEI YA BIDHAA KAMA HAUNA MPANGO WA KUNUNUA
-
Ikitokea bei ikawa ndogo utanunua tu.
0 Maoni