KUENDELEZA MAONO AU KAZI NJEMA ZA WAZAZI WAKO


 Faraja Gasto

Wajibu mmojawapo wa watoto ni kuendeleza mambo mema yaliyofanywa na wazazi au kutekeleza mipango mizuri iliyoachwa na wazazi au kuendeleza maono mema ya wazazi BAADA YA WAZAZI KUFARIKI.

 

Wapo wazazi ambao wanafariki huku wameacha ujenzi wa nyumba haujakamilika, wapo wanaofariki huku wakiwa wameacha makampuni, mashirika, taasisi n.k, wapo wanaofarariki huku wameacha mipango na maono mazuri, SHIDA INAKUJA PALE KUNAPOKOSEKANA MTOTO AU WATOTO WA KUENDELEZA MAONO AU KAZI ZA NJEMA ZA WAZAZI.

 

(MWANZO 26:18)

Ibrahimu alipofariki aliacha visima, visima vile vilifukiwa na wafilisti lakini ulifika wakati MTOTO WA IBRAHIMU (ISAKA) AKARUDI KUVICHIMBUA TENA.

 

Ninachotaka uone hapo ni kwamba "sio vema kuacha maono au kazi njema zilizoanzishwa na wazazi wako zikafa, ni heri kuziendeleza kwa kuwa zinaweza kuleta manufaa kwako, kwa ndugu zako, kwa jamii, kwa taifa na dunia"

Tujenge utamaduni wa kuendeleza maono, mipango au kazi njema zilizoachwa au zitakazoachwa na wazazi wetu.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni