Kuchukua
au kulala na mke wa mtu ni jambo lenye madhara makubwa japo si wengi wanafahamu
ndio maana Mungu amekataza hata kumtamani mke wa mtu (KUTOKA 20:17b)
Dhambi
ya kulala na mke wa mtu, Yusufu aliita UBAYA MKUU (MWANZO 39:6-9)
Mfalme
Abimeleki alipochukua mke wa mtu, MUNGU ALIYAFUNGA MATUMBO YA WATU WA NYUMBA YA
ABIMELEKI ILI WASIZAE WATOTO, TENA MUNGU ALIKUSUDIA KUWAANGAMIZA WOTE (MWANZO
20:1-18) Japo Abimeleki hakulala naye lakini kumchukua mke wa mtu lilikuwa kosa.
(2
SAMWELI 11:2-27)
Mfalme
Daudi alichukua mke wa mtu akalala naye akabeba mimba kisha Daudi akamuua mume
wa yule mwanamke, jambo lile lilisababisha nyumba ya Daudi ikaandamwa na
matatizo makubwa, soma (2 SAMWELI 12:11-18) soma 2 SAMWELI sura ya 13, 14, 15
n.k
Angalizo
1.
Mwanamke aliyeachwa na mumewe sio mjane, usilale naye kwa kuwa bado ni mke wa
mtu.
2.
Usimuue mume wa mtu ili uchukue mkewe.
3.
Haimaanishi ni halali kuchukua mume wa mtu.
4.
Usimuachanishe mume na mke ili uchukue mkewe.
0 Maoni