Faraja Gasto
(Waefeso 6:18-20)
Mtume Paulo alitoa wito kwa waefeso ili wamuombee
apewe usemi afumbue kinywa chake ili ahubiri kwa ujasiri siri ya injili.
(Luka 22:31-32)
Shetani alitamani kuwapepeta kama ngano wanafunzi
wa Yesu, Yesu alimtegemeza Petro kwa maombi ili imani yake isitindike.
(3 Yohana 1:1-4)
Mtume Yohana alimtegemeza kwa maombi mtumishi wa
Mungu Gayo ili afanikiwe katika mambo yote, awe na afya kama roho yake
ifanikiwavyo.
NB: Tusiishie kuwategemeza watumishi kwa kuwapa
vitu, tuwape vitu pia tuwategemeze kwa njia ya maombi.
-->Waombee watumishi wapewe usemi ili wahubiri
kwa ujasiri siri ya injili.
-->Waombee imani zao zisitindike.
-->Waombee wafanikiwe kiroho na kimwili.
-->Ombea ndoa za watumishi wa Mungu.
-->Waombee Mungu awaponye waliojeruhiwa mioyo.
Msisitizo: Ruhusu Roho wa Mungu akuongoze kuwaombea
watumishi wake.
0 Maoni