Hili
ni somo maalumu kwa ajili ya watumishi wa Mungu hususani walioitwa na Mungu katika utumishi.
Jambo
mojawapo la muhimu sana katika maisha ya utumishi ni KUJIPAMBANUA.
Kujipambanua
ni kufahamu au kuwa na uhakika MUNGU AMEKUITA KUFANYA NINI, kumbuka Mungu
hajakuita kufanya kila kitu bali lipo jukumu au majukumu ambayo anataka
uyatekeleze.
(Mathayo
4:18-20)
Yesu
alipowaita Petro na Andrea aliwaambia "nifuateni nami nitawafanya kuwa
wavuvi wa watu"
Kwa
hiyo Petro na Andrea walijipambanua wameitwa kuwa wavuvi wa watu kwa kuwa
aliyewaita aliwaambia amewaita kufanya nini.
NB:
Kile ambacho Mungu amekuitia ndicho atakachokufundisha kukifanya, Mungu hawezi
kukufundisha kile ambacho hajakuita kukifanya ndio maana alipowaita Petro na
Andrea aliwaambia wamfuate atawafanya (atawafundisha) kuwa wavuvi wa watu.
(Yohana
1:19-27)
Yohana
alipoulizwa wewe ni nani? alijibu kuwa "mimi ni sauti ya mtu aliaye
nyikani"
-Yohana
alijipambanua kuwa ameitwa kutangulia mbele ya Yesu kumtengenezea njia.
Je!
Wewe mtumishi umeitwa kufanya nini?
Msisitizo:
sio vema kudumu katika maisha ya utumishi bila kuwa na uhakika Mungu amekuita
kufanya nini au bila kuwa na uhakika Mungu anataka ufanye nini.
Usipokuwa
na uhakika umeitwa kufanya nini utajikuta unafanya chochote lakini fahamu kuwa
Mungu hajakuita ufanye chochote.
(Warumi
1:1)(1 Wakorintho 1:1)(Waefeso 1:1)
Ukisoma
maandiko hayo utaona mtumishi wa Mungu Paulo akijipambanua kuwa aliitwa kuwa
mtume wa Yesu Kristo.
(Hesabu
16:28)
Musa
alijipambanua kuwa ameitwa kuwaongoza wana wa Israeli, hata watu baadhi
walipomuinukia hakubabaika kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa aliitwa kuwaongoza
wana wa Israeli.
NB:
Ikitokea vita wakati unatembea katika wito wako utaona Mungu akikupigania
lakini ukikutana na vikwazo halafu hauoni msaada wa Mungu uwe na uhakika kuwa
Mungu hakukuita kufanya hicho unachofanya ndio maana haupati msaada wake.
Hivyo
basi kuliko kuendelea kujitaabisha ni heri umuulize Mungu amekuita kufanya
nini, USIJITAABISHE KUFANYA MAMBO AMBAYO MUNGU HAJAKUITA KUYAFANYA.
Mathayo
4:18-22
Yesu
alipowaita Petro na Andrea aliwaambia "nifuateni nami nitawafanya kuwa
wavuvi wa watu"
Lakini
alipowaita Yakobo na Yohana hakuwaambia maneno aliyowaambia Petro na Andrea.
NB:
Mungu anaweza kukuita lakini asikwambie hapohapo amekuita kufanya nini lakini
kadiri utakavyotulia miguuni pake atakuambia alichokuitia, hivyo basi usianze
kujivika vyeo, majina n.k tulia miguuni pa Bwana atakuambia alichokuitia, pia
Mungu anapoita watu huwapatia kazi tofautitofauti (japo wanaweza kuitwa kwenye
ofisi moja lakini majukumu yatatofautiana) kwa hiyo usidharau kazi aliyokupa
Mungu, usifanye kazi walizopewa wengine tena usitake kuiga jinsi wengine
wanavyotumika (usitake kufanana na wengine.
0 Maoni