JINSI YA KUKAA NDANI YA YESU NA FAIDA ZA KUKAA NDANI YA YESU

UTANGULIZI

Yesu alitoa wito kwa wanafunzi wake na watu wote ambao wanamuamini kuwa wakae ndani yake naye ndani yao.

(Yohana 15:4)

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.”

 

 

JINSI YA KUKAA NDANI YA YESU

1.     Okoka (mwamnini Yesu)

(1 Yohana 3:9)

Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.”

 

(1 Yohana 4:15)

Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.”

Ili uweze kukaa ndani ya Yesu lazima uokoke au umwamini Yesu.

2.     Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yako na uzishike amri zake

(1 Yohana 2:24)

Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.”

 

(1 Yohana 3:24)

Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.”

 

3.     Kula mwili wa Yesu na kunywa damu yake (shiriki meza ya Bwana)

(Yohana 6:56)

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.”

 

4.     Kupendana sisi kwa sisi (upendo katika jamii ya waaminio)

(1 Yohana 4:12-13, 16)

“12. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13. Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. 16. Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.”

 

 

 

BAADHI YA FAIDA ZA KUKAA NDANI YA YESU

1.     Utakuwa hai kiroho

(Yohana 6:57)

“56. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.”

 

2.     Utapata uwezo wa kushinda dhambi

(1 Yohana 3:6)

“Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala

hakumtambua.”

 

3.     Utakuwa na uwezo wa kumzalia Mungu matunda, huduma yako itamzalia Mungu matunda pia ukristo wako utamzalia Mungu matunda.

Kumzalia Mungu matunda ni wajibu wa kila aliyemwamini Yesu, tutaweza kumzalia Mungu matunda  endapo tutakaa ndani ya Yesu.

 

(Yohana 15:4)

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.”

 

4.     Mungu atayajibu maombi yako, lolote utakalomuomba atakupa.

(Yohana 15:7)

“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

 

 

Chapisha Maoni

0 Maoni