Watu wengi katika ulimwengu huu wamepoteza uwezo wa aina mbalimbali
kutegemeana na sababu mbalimbali, wengi wamepoteza aina mbalimbali za uwezo
kama vile
v Uwezo wa
kukumbuka mambo
v Uwezo wa
kusikia
v Uwezo wa
kuona
v Uwezo wa
kuzaa
v Uwezo wa
tendo la ndoa
v Uwezo wa
kutembea n.k
Wengine wamefanya jitihada mbalimbali ili
kurejesha uwezo huo lakini imeshindikana kabisa, ndio maana nakuletea somo hili
kuhusu UWEZO WA JINA LA YESU KATIKA KUKUREJESHEA UWEZO ULIOPOTEZA.
Biblia inasema ni jina moja tu ambalo
tumepewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ni jina la YESU (Matendo ya mitume
4:12)
“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana
hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi
kuokolewa kwalo.”
(Yohana
1:12)
“Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
Biblia
inasema kuwa wote waliomwamini Yesu WALIPEWA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU
KUPITIA JINA LA YESU TU. Kumbe jina la Yesu lina uwezo wa kutupa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu endapo mtu ataliamini hilo jina.
IKO
HIVI: Kama jina la Yesu linawapa watu uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, wale
wanaoliamini basi uwe na uhakika jina la Yesu linaweza kumpa mtu uwezo wa aina
yoyote anaouhitaji endapo ataliamini tu hilo jina la Yesu.
(Matendo
ya mitume 3:6)
“6. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu,
lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa
jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
7. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake
vikatiwa nguvu. 8. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia
ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.”
Tunaona
kuwa jina la Yesu lilimpa huyo kiwete uwezo wa kutembea, nami nakuhakikishia
kwamba jina la Yesu linaweza kukupa uwezo wowote au kukurejeshea uwezo wowote
ulioupoteza endapo utaliamini hilo jina.
USHUHUDA
Rafiki
yangu Fulani alinipeleka kumuombea mama mmoja aliyekuwa amerogwa mguu wake,
mguu ulikuwa umevimba sana na una kidonda, walijaribu kupata matibabu hospitali
mbalimbali lakini ikashindikana kwa kuwa ugonjwa ulikuwa hauonekani kwenye
vipimo vya hospitali, alipokata tamaa akaamua kurudi nyumbani kusubiri kufa kwa
kuwa alikuwa hawezi tena kutembea.
Yule
rafiki yangu aliponipeleka pale nikaanza kumueleza Yule mama habari za Yesu,
kwa muda alikataa kumwamini Yesu akataka nimwombee tu aone hali itakuwaje ndipo
atamwamini Yesu lakini kabla sijaanza kuomba akakubali kumwamini Yesu,
nikamuongoza sala ya kumkiri Yesu halafu nikaanza kuomba.
Baada
ya siku kama mbili ule uvimbe ukaanza kupungua na kile kidonda kikaaza kukauka,
baada ya siku kadhaa Yule mwanamke akaanza kutembea, akamuona Mungu,
akashuhudia uwezo wa jina la Yesu.
Nimekueleza
ushuhuda huo ili uone nguvu zilizomo katika jina la Yesu, jina la Yesu linaweza
kukupa uwezo ulioupoteza, jina la Yesu linaweza kukupa uwezo ambao haukuwa nao
endapo utaliamini hilo jina.
HITIMISHO
Ni
muhimu sana ufanyike mwana wa Mungu kupitia kumwamini Yesu, kama uko tayari
kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, sema maneno haya.
Mungu Baba nakushukuru kwa upendo wako kwa ajili ya
ulimwengu, ninamkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa ulimwengu ninaamini kuwa
Mungu Baba ulimfufua Yesu katika wafu, ninaomba unisamehe dhambi zangu zote
nioshe kwa damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani kwa kuwa nimerejea kwako
mimi niliyekuwa nimepotea, Asante Baba kwa kunisamehe na kunisafisha, asante
kwa kuwa jina langu umeliandika kwenye kitabu cha uzima.
Baada ya kusema maneno hayo tayari umeokoka,
nameinitapenda kuwasiliana nawe ambaye umeokoka, tuwasiliane kwa namba za simu _+255767955334
au +255625775243
Pia litumie jina la Yesu katika maombi yako, ikiwa kuna
uwezo unautaka hebu muombe Mungu akupe au akurejeshee kwa jina la Yesu.
0 Maoni