Faraja Gasto
(1 Petro 5:8)(Yohana 10:10)
Bwana Yesu asifiwe, napenda kukuletea somo hill
ambalo halitakuacha kama ulivyo.
LENGO LA SOMO: Ili usimpe Ibilisi nafasi (Waefeso
4:27)
Ukisoma Biblia utagundua kuwa shetani huwa anatafuta
watu (1 Petro 5:8)
“Mwe
na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze.”
DIRA YA SHETANI NA UFALME WAKE (VISION)
Kuiba, kuua na kuharibu (Yohana 10:10)
DHAMIRA YA SHETANI NA UFALME WAKE (MISSION)
Kutafuta NAFASI ya kuiba, kuua na kuharibu (Waefeso
4:27)
Kwa hiyo unatakiwa kufahamu kuwa kazi zote za
shetani na ufalme wake zinaongozwa na dira ya ufalme wake ambayo ni kuiba, kuua
na kuharibu.
Shetani anapomtafuta mtu huwa anakusudia kuiba,
kuua na kuharibu, mapepo na wachawi wanapomshambulia mtu huwa wanakusudia
kuiba, kuua na kuharibu ndio maana tunajifunza somo hili ili usije ukajikuta
umempa shetani NAFASI (Waefeso 4:27)
(Ayubu 1:6-12)
Mungu alipomuuliza shetani "unatoka wapi"
ona jibu shetani alilojibu "natoka KUZUNGUKAZUNGUKA na KUTEMBEA TEMBEA
HUKU NA KULE" Shetani alipojibu hivyo haina maana kwamba yeye in
mzururaji, yeye anazungukazunguka ili kutafuta NAFASI ya kuiba, kuua na
kuharibu ndio maana Mungu alipompa kibali cha kumshughulikia Ayubu, shetani
aliharibu Mali za Ayubu pia akaua watoto wa Ayubu. Hili ni somo muhimu sana la
kukusaidia kushinda na zaidi ya kushinda.
FAHAMU MAMBO HAYA
1. Shetani hamtafuti kila mtu Bali anawatafuta ambao
hajawakamata, iko hivi hakuna mtu ambaye anaweza kutafuta alichokipata, Bali
kila mtu anatafuta kile ambacho hajakipata hata shetani anawatafuta watu ambao
hajawapata. Kwa hiyo kama umeokoka fahamu kuwa shetani anakutafuta usiku na
mchana na kama haujaokoka fahamu kuwa shetani amekuweka kwenye himaya take sasa
kumbuka ile dira ya shetani na ufalme wake niliyokuonyesha pale juu, fanya
maamuzi ya kuokoka.
2. Shetani huwa anaanza kumtafuta mtu tangu akiwa
tumboni, yaani vita ya shetani na mwanadamu inaanza toka mwanadamu akiwa
tumboni ndio maana si ajabu kuona watoto wanafia tumboni au wengine wanazaliwa
wamekufa na wengine wanazaliwa wakiwa mabubu au viziwi au viwete au vipofu,
wengine wanazaliwa wakiwa wendawazimu, wengine wanazaliwa na vichwa vikubwa n.k
hiyo ni vita ya shetani wala sio mapenzi ya Mungu iwe hivyo, usalama ni kuokoka
na kukaa kwenye ufalme wa Yesu.
(Matendo ya mitume 3:1-2)
Ukisoma hilo andiko utaona kuwa huyo mtu alikuwa
kiwete tangu tumboni hatimaye akazaliwa akiwa kiwete, ndugu usifanye mchezo na
shetani hana huruma hata kidogo kama haujaokoka hebu okoka, zipo faida nyingi
za kuokoka, ukisoma Biblia utagundua kuwa shetani alipofukuzwa mbinguni alikuja
akiwa amejaa GHADHABU kwa hiyo anatamani kuiba, kuua na kufanya uharibifu kila
kukicha.
3. Shetani yuko tayari kulipa gharama yoyote ili
ampate mtu mmoja anayemtaka
(Mathayo 4:8-9)
Shetani aliwahi kumwambia Yesu kuwa
"ukinisujudia" nitakupa hizi milki unazoziona.
Fahamu kuwa shetani anaweza kumpa mtu Mali lakini
lengo lake ni kumuua huyo mtu au kuharibu kabisa maisha take ndio maana wote
waliopewa utajiri na shetani hawana amani kabisa hawawezi kusema lakini
wanaumia, wengine hawalali vitandani wanalala chooni au makaburini, wengine
hawavai Viatu bali wanavaa ndala yaani shetani ni msumbufu hujawahi kuona ndio
maana kuna wengine wamepata ajira kwa kutoa rushwa ya ngono, wengine wamefaulu
vyuoni au mashuleni kwa kuuza miili yao, wao wanaona kawaida lakini shetani
anawatamani, Kama haujamwamini Yesu mwamini leo kwa kuwa kuna raha huku kwa
Yesu.
Shetani anawatafuta watu kwa njia mbili tu.
1.
Anatafuta mtu MOJA KWA MOJA (direct)
2.
Anatafuta mtu kwa njia ambazo SIO ZA MOJA KWA MOJA (indirect)
NJIA
YA MOJA KWA MOJA
Shetani
anaweza kumtafuta mtu kwa kumfuata mtu moja kwa moja yaani shetani anaweza kuja
yeye mwenyewe kwa mtu.
(Mathayo
4:1-11)
Shetani
alimfuata Yesu moja kwa moja akaanza kumshawishi ili akubaliane nae.
KWA
NJIA ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA
Shetani
anaweza kuwatumia watu kwa mfano mke wako, mume wako, mazingira, watoto wako,
ndugu, jamaa na marafiki.
(Mwanzo
3:1-7)
Shetani
alimtafuta Adamu ila hakwenda moja kwa moja kwa Adamu bali alimtumia mke wa
Adamu, make wa Adamu alipoingilika akala tunda lakini hauoni akifumbuliwa macho
lakini Adamu alipoingilika akala tunda ghafla wakafumbuliwa macho wote wawili
anaweza ukajiuliza ni kwa mini iwe hivyo? ni kwa sababu Adamu ndiye alipewa
maagizo (yeye ndiye mbeba maono) alipokula tu mambo yakaharibika.
(Mathayo
16:21-22)
Shetani alimtafuta Yesu kupitia
Petro, akaweka mawazo hasi ndani ya Petro ili amshawishi Yesu lakini Yesu akajua
ni shetani akamkemea.
Hizi ni baadhi ya dalili au ishara kuwa shetani
anakutafuta
1.
MAKWAZO
Shetani
huinua watu wa kukukwaza.
2.
KUKOSA NJAA YA NENO LA MUNGU
Ukiona
unashindwa kusoma Biblia, au unaona wahubiri wanachelewa kumaliza mahubiri au haupendi
mafundisho fahamu kuwa hizo ni dalili mbaya.
3.
KUONGEZEKA KWA USHAWISHI WA KUTENDA DHAMBI
Kwa
mfano kushawishiwa kuzini, kuiba, kuabudu miungu n.k
4.
MAWAZO MABAYA
Kati
ya mambo yanayowasumbua watu, kitu kimojawapo ni mawazo mabaya, mawazo mabaya
yanaletwa na shetani ili kumfanya mtu afanye dhambi.
5.
KUKATA TAMAA YA KUOMBA
Kukata
tamaa ya kuomba ni kuacha kuomba, hiyo ni dalili ya kutafutwa na shetani.
6.
KUTOKWENDA IBADANI
Ukiona
unaanza kukwepa kwenda ibadani fahamu kuwa shetani anakusogelea.
Hizo
ni baadhi ya ishara au dalili za kunyemelewa na shetani, Mungu akubariki na
akupe nguvu ya kutendea kazi.
0 Maoni