Faraja Gasto
0767955334
“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana
umekuzukia”
(Isaya 60:1)
Utangulizi
Hayo
maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu cha (Isaya 60:1), walikuwa wanaambiwa wana
wa Israeli kuwa waondoke waangaze kwa kuwa nuru yao imekuja.
NURU
NI MWANGA ambao unatakiwa kuangaza.
KAZI MBILI ZA NURU
11. ni kumuangazia mtu ili asijikwae
22. kuondoa giza.
AINA KADHAA ZA NURU
1.Nuru
ya jua 2.Nuru ya mwezi 3.Nuru ya umeme 4. Nuru ya radi 5.Nuru ya taa (chemli) 6.Nuru ya koroboi
Hizo
ni baadhi ya Nuru.
NURU KATIKA AGANO JIPYA
(Yohana
1:9) – YESU NI NURU
Biblia
inasema Yesu ni nuru ambaye anamtia nuru kila mtu anayemwamini, kwa hiyo kama
umemwamini Yesu fahamu kuwa wewe una nuru na wewe pia ni nuru.
(Mathayo
5:14-16) – SISI WAKRISTO NI NURU
Biblia
inasema sisi ni nuru ya ulimwengu, kwa hiyo NURU YETU INATAKIWA KUANGAZA MBELE
YA WATU
JUKUMU LETU SISI WAKRISTO
Jukumu
letu kubwa sisi wakristo ni KUANGAZA kwa kuwa sisi ni nuru ya ulimwengu, kwa
hiyo tuna kazi ya kuwaangazia watu wasijikwae au wasianguke na pia tuna kazi ya
kuondoa giza kwa kuwa kazi mojawapo ya nuru ni kuondoa giza.
ILI NURU YETU IANGAZE LAZIMA TUFANYE
YAFUATAYO
(MATHAYO 5:15)
Biblia
inasema watu hawawashi taa na kuiweka chini bali wanaiweka juu ILI IWAANGAZIE
WATU waliomo ndani, hiyo ni sawa na kusema tunapompokea Yesu ambaye anatutia
nuru lazima tufanye yafuatayo
1.Kuwaambia wengine habari za Yesu
(Nuru)
Unapoaambia
wengine habari za Yesu ni sawa na kuwapelekea watu nuru kwa kuwa wote ambao hawana
Yesu wako kwenye giza, unapowaambia habari za Yesu unakuwa unawapa nuru ili
wasitembee kwenye giza.
Biblia
inasema Yohana mbatizaji aliishuhudia ile NURU ambaye ni Yesu yaani maana yake
ni kwamba Yohana aliwaeleza watu habari za Yesu ambaye ni nuru ili watu wapate
kumuamini, soma (YOHANA 1:6-7)
2.Matendo yetu yanatakiwa kuwafanya
watu wamtukuze Mungu
(MATHAYO 5:16)
Biblia
inasema NURU YETU IANGAZE ili watu WAPATE KUYAONA MATENDO YETU MEMA wamtukuze
Mungu.
Kwa
hiyo sisi kwa kuwa ni nuru ya ulimwengu tunatakiwa kuangaza kwa njia ya matendo
yetu mema ili watu watakapoyaona matendo yetu mema wapate kumtukuza Mungu.
Matendo
yetu yakifanyika nuru lazima watu watakuja kwa Yesu na pia lazima watu
watatamani kusikia habari za Yesu.
(1
PETRO 3:1-5)
Biblia
inasema wanawake wa zamani walijipamba kwa matendo mema, matendo mema yana
nguvu ya kuwavuta watu waje kwa Yesu Kristo hata kabla hawajahubiriwa habari za
Yesu, soma (1 PETRO 3:1)
Mwisho
Sisi
wakristo tuna wajibu wa kwenda kuangaza kwa kuwa sisi ni Nuru na pia tunaye
Yesu aliye nuru.
Tunapoangaza
tunawafanya watu wasijikwae, wasitembee gizani kwa kuwa mahali palipo na nuru
lazima giza litatoweka.
0 Maoni