FAHAMU MAMBO YANAYOWAFANYA WATU WAFANYIKE KUWA WATEJA WA BIDHAA AU HUDUMA FULANI

Faraja Gasto
Lengo la makala: Kukufahamisha mambo yanayomfanya mtu afanye maamuzi ya kipi anunue na kipi asinunue, kipi atumie na kipi asitumie.

 *Utangulizi*
Ili uweze kufanikiwa na kufanya vizuri katika biashara ni muhimu ufahamu mambo yanayowafanya watu wawe Wateja wa bidhaa au huduma fulani.

 *MAMBO HAYO NI HAYA*
1.Ladha, muonekano, uzoefu na taarifa zilizotengeneza Mapendeleo (preferences)
--Bidhaa yoyote uliyowahi kuitumia au unayoitumia, unaitumia kwa sababu ya kuipenda,   kipo kilichokuvutia ukajikuta umeipenda hiyo huduma au bidhaa yawezekana ni ladha ya bidhaa, yawezekana umewahi kuitumia bidhaa au huduma kama hiyo kwa hiyo umeizoea,  yawezekana ni muonekano wa bidhaa nakadhalika.

2.Ubora wa huduma au bidhaa na gharama ya bidhaa au huduma
----Ni watu wachache wanaotumia huduma au bidhaa fulani kwa kigezo cha ubora,  wengi wanatumia huduma fulani au bidhaa fulani kwa sababu ina gharama nafuu,  yaani kwao ubora sio ajenda bali gharama za bidhaa au huduma.
Ubora wa huduma au bidhaa unapimwa na vitu vingi ikiwemo GHARAMA ZA HUDUMA AU BIDHAA,  kama bidhaa ina bei ndogo maana yake ubora wa bidhaa ni mdogo (kinyume cha hii kauli ni sahihi)

3.Huduma nzuri kwa mteja (customer care)
----Wapo watu wanaotumia bidhaa au huduma fulani kwa sababu walipewa huduma nzuri,  walihudumiwa vizuri.
Huduma kwa wateja ina nguvu kubwa ya kuvuta wateja wengi kwenye biashara.

4.Mahali bidhaa au huduma ilipo (distance&location)
-----Kuna watu wanatumia bidhaa au huduma fulani kwa sababu ya eneo  ambalo bidhaa ipo au huduma ipo,  watu wengi wako tayari kununua bidhaa au kutumia huduma fulani kwa kigezo cha umbali na eneo,  kama bidhaa iko karibu au kama huduma iko karibu basi watatumia hiyo bidhaa na hiyo huduma kwa sababu iko karibu nao.
Kwa hiyo unapofanya biashara ni muhimu uzingatie suala la eneo na umbali kutoka kwa wateja mpaka kwenye eneo lako la biashara.

5.Utofauti aliouona mteja kwenye bidhaa yako au huduma yako
---Utofauti unaoonekana kati ya bidhaa na bidhaa na kati ya huduma na huduma una nguvu ya kuvuta wateja kwenye biashara yako.
Zipo njia nyingi za kutengeneza utofauti wa bidhaa zako na za wengine au utofauti wa huduma zako na za wengine, hizi ni njia baadhi
1.Vifungashio (packages)
2.Muonekano (appearance)

Kwa ushauri wa masuala ya kibiashara,  uchumi na maendeleo,  wasiliana nami kwa 0767955334 Waweza kupiga simu au kutuma ujumbe.

Chapisha Maoni

0 Maoni