UWEKEZAJI

Faraja Gasto

Kimsingi hakuna anayependa kuona fedha zake zinapotea bure, hakuna anayependa kupanda mbegu nyingi halafu akavuna kidogo, hakuna anayependa kutumia nguvu nyingi halafu asipate matokeo aliyoyatarajia.
Kama haupendi hayo mambo niliyotaja hapo juu basi una uhitaji wa kujifunza somo la UWEKEZAJI (investment)
Swali kubwa walilonalo watu wengi wanaotaka kuwekeza ni hili
" niwekeze wapi ili nipate faida (nifanye kitu gani ambacho kitanipa faida)

UWEKEZAJI - Kuweka fedha zako au nguvu zako  mahali fulani ukiwa na lengo la kupata faida.

Kila mjasiriamali ni MWEKEZAJI ambaye ana lengo la kupata faida ya uwekezaji wake.

AINA KADHAA ZA UWEKEZAJI
1.Uwekezaji katika soko la HISA
-->Kwa mfano kuuza na kununua hisa

2.Uwekezaji unaolenga kutatua matatizo ya kijamii n.k
--->Kwa mfano usafirishaji n.k

3.Uwekezaji unaolenga kutoa huduma za kijamii
--->Kuanzisha mgahawa, maabara, kuuza nguo n.k

4.Uwekezaji kwenye kilimo na ufugaji
-->Kwa mfano ukulima na ufugaji (livestock keeping)

 UWEKEZAJI UNA MATOKEO YA AINA MBILI
1.Faida (profit)
2. Hasara (loss)
Hakuna mtu yeyote ambaye anawekeza kwa lengo la kupata hasara, ila hasara ni matokeo.

ILI KUEPUKA HASARA KATIKA UWEKEZAJI LAZIMA UFIKIRI MAMBO KADHAA

1.Wapi unataka kuwekeza?
2.Muda gani unataka uwekeze na utatumia muda gani kuwekeza?
3.Unawekeza kwenye mazingira yapi?
4.Unazijua taratibu muhimu za kisheria kabla ya kuwekeza?
--->Kwa mfano suala la leseni n.k
Ukitathmini kwa kina kuhusu hayo maswali manne, majibu yatakusaidia kufanya maamuzi mazuri ya uwekezaji.
Kwa hii makala fupi naamini umejifunza kitu. 

Chapisha Maoni

0 Maoni