Faraja Gasto
Utangulizi
Tunapozungumzia
kupanua soko hatuwezi kuepuka kuzungumzia mambo makuu mawili
1.Uhitaji (Demand)
2.Usambazaji (Supply)
àHayo
ni mambo ambayo unatakiwa kuyafikiria kabla ya kufikiria kupanua soko
Kupanua soko la
bidhaa inahitaji MIKAKATI(strategies)
Ijulikane kuwa kupanua
soko haina maana ni kuongeza ukubwa wa eneo unalofanyia biashara bali ni
kuifanya biashara yako ijulikane sehemu tofauti tofauti hatimaye upate wateja
wengi zaidi katika biashara yako.
Ila kabla ya kuwaza
kutanua soko lazima mfanyabiashara awaze UHITAJI WA BIDHAA (Je! Bidhaa yake
inapofika mahali fulani itanunuliwa na watu wa eneo husika?), nimesema hivyo kwa
sababu kupanua soko ITAHITAJI GHARAMA,
kwa hiyo gharama utakazotumia kutanua soko lako lazima uhakikishe
zinarudi. Pia watu wengi huwa hawatumii kitu ambacho hawakifahamu vema
(hawajakizoea).
Mbinu
kadhaa za kupanua soko
1.Tangaza
biashara yako au bidhaa zako (Advertising your products)
-Zipo njia nyingi za
kutangaza biashara yako kwa mfano unaweza kuitangaza kwa kuwaambia watu walio
karibu na wewe au kwa njia ya mtandao wa intaneti, redio,
televisheni, P. A (public Attention) n. k, itategemea mfuko wako umekaaje ndio maana
nilikuambia kutanua soko ni suala la mkakati na linahitaji gharama.
Nikupe mfano,
mitandao ya simu (Vodacom, Tigo, Airtel n. k), huwa wanawatumia meseji wateja
wao ili kuwapa taatifa za ofa mpya n. K hizo ni mbinu za kutoa matangazo
wanazozitumia ili wewe mtumiaji wa mtandao huo uvutike kununua hicho kifurushi
n.k, kwa lugha ya kibiashara wanakuwa wanafanya MARKETING.
2.Tengeneza
mabalozi wa biashara yako sehemu mbalimbali
-Nianze kwa kuupa
mfano, naamini katika mtaa unaoishi unaona kuna mawakala wa mitandao kama vile
mawakala wa Vodacom, Tigo, Halotel n.k, hizo kampuni za simu zinalenga kupanua
soko lake kwa kuleta huduma karibu na wateja. Ikiwa uchumi wako uko vizuri
unaweza na wewe ukapanua biashara yako kwa nia hii inayotumiwa na makampuni
haya ya simu.
-Namna rahisi ya kutengeneza mabalozi wa
biashara yako ni kwa njia ya OFA (ila lazima uwe na tahadhari katika kutoa ofa
usitoe ofa ovyoovyo jifunze kuwapa ofa wateja wa kudumu)
Nikupe mfano, kuna
watu wakisikia Tigo wametoa ofa utashangaa kesho anatafuta line ya Tigo, ofa
ikiisha si ajabu akatupa line, kuna watu
wakisikia Voda wana ofa utaona anatafuta line ya voda, HAO SIO WATEJA WA KUDUMU, kwa hiyo katika kuwapa ofa lazima uwe na
tahadhari ili wasiishushe biashara yako.
Sababu
mojawapo kwa nini ofa zinatolewa
Ni kwa sababu
anayepewa ofa huwa anajikuta (automatically) amekuwa balozi au wakala wa huyo
mtoa ofa, lazima atawaambia wengine kuhusu hiyo ofa, wengine
wakiisikia lazima watachangamkia fursa.
3.Hakikisha una
bidhaa zenye bei tofauti, ikiwezekana ziwe na muonekano au ladha tofauti
--Ni
muhimu kufanya hivyo kwa sababu
(a)Uwezo wa kiuchumi
wa wateja unatofautiana
(b)Wateja wanataka
ladha tofauti au bidhaa za aina tofautitofauti
Kwa mfano kampuni ya
Coca cola inatengeneza svinywaji balimbali kama Coca cola, Fanta, Sprite n.k
Wanafanya hivyo ili
kupanua soko lao.
0 Maoni