Faraja Gasto
Utangulizi
Sula la kupata mtaji
limekuwa kilio cha kila mwenye WAZO la ujasiriamali. Lakini ukweli ni kwamba
shida sio mtaji shida ni MFUMO WA KUFIKIRI.
Watu wengi wanapokuwa
na mawazo ya biashara huwa hawakai chini na kutafakari kuhusu mambo muhimu sana
kabla ya kuanza biashara, kuna watu wanalia hawana mitaji lakini ukweli ni
kwamba mitaji wanayo ila hawajui kama wanayo mitaji.
Njia rahisi za kupata
mtaji wa biashara
1.Badili ulichonacho
kuwa mtaji (Cash equivalent)
“Ulichonacho
kinatosha endapo UTAFIKIRI vya kutosha”
--Ask.
David Oyedepo—
Nina uhakika una
simu, una mavazi mazuri, una vifaa vya ndani vizuri. Vibadili hivyo kuwa fedha
ya mtaji, njia mojawapo ya kuvibadili kuwa fedha ni KUUZA.
Ni vema ufahamu kuwa
kuna wakati unatakiwa kuchukua hatua za hatari (risk taking) kwa kuwa kuuza
vitu vyako ni kufanya maamuzi magumu ili yana faida kwa baadaye maana fedha
utakazotumia kuwekeza kwenye biashara zitazaa na hatimaye utavinunua tena
ulivyouza.
2. Washirikishe WAZO
LAKO watu wa karibu na wewe, wale unaowaamini.
“Ukitaka
kwenda haraka nenda peke yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako”
--Msemo
wa wahenga—
Nakumbuka wakati fulani
niliona katika mtaa Fulani kuna fursa ya kuweka duka la kuuza vifaa vya shule
n.k (stationery) wakati huo nilikuwa bado niko masomoni, nilipomaliza nikaanza
kutafuta pesa ya kununua vifaa, ikabidi nikope kwa ndugu yangu shilingi laki
moja, kasha nikakopa kwa mjomba wangu laki moja na elfu thelathini, baada ya
hapo nikatfauta tarakilishi ya kukodi(computer), nikatafuta chumba nikapata cha
laki na nusu ikabidi nizungumze na mwenye chumba akakubali nikampa kwanza
shilingi laki moja kisha ile pesa niliyokuwa nayo nikatafuta mahali pa kupata
mashine ya kutolea vivuli (photocopy), na kuprinti (printer), nikatafuta mahali
Fulani pesa nikanunua baadhi ya vifaa. Nilipomshirikisha mjomba wangu fulani
hilo wazo akaniambia “dah mbona haukusema mapema kama unataka kufanya hiyo
biashara, kama ungesema mapema ungeweza kupata vifaa maana kuna mtu fulani
alikuwa na hivyo vifaa ameacha hiyo kazi amesafiri kwenda nje ya nchi angeweza
kukuuzia kwa bei nafuu”
Nilijilaumu sana kwa
nini sikumwambia hilo wazo, ninachokufundisha hapa ni kwamba unapokuwa na wazo
la biashara na hauna pa kuanzia jifunze kuwashirikisha watu unaowaamini ambao
wako karibu na wewe hata kama hawatakupa pesa, watakupanua ufahamu na kukupa
mawazo ya ziada. Ilifika hatua biashara yangu ikayumba lakini kanisa nilipokuwa
nasali likaniazima pesa ya kuendeleza biashara yangu.
3.Kopa fedha kwa watu
walio karibu na wewe kabla ya kukopa kwenye taasisi (financial institutions)
-Ni
heri kukopa kwa watu walio karibu na wewe
-Kukopa fedha kwenye
taasisi linatakiwa kuwa suala la mwisho endapo unaona haina jinsi.
ANGALIZO: Unapokopa
kwenye taasisi hakikisha hiyo fedha haifiki nyumbani, nenda moja kwa moja
ukanunue bidhaa, ukalipie pango la biashara n.k. Nakuambia hivyo kwa sababu ya
uzoefu nilionao, watu wengi wanapofika na pesa za mkopo nyumbani ghafla
mahitaji huwa yanaanza kuinuka kwa hiyo mkopaji anajikuta pesa aliyonayo
haitoshi kwa kuanzia biashara.
4.Jiwekee malengo ya
kupata mtaji ndani ya muda fulani kisha anza kuweka akiba
à Kama
una malengo ya kupata mtaji wa sh milioni moja hakikisha unaweka MUDA wa kupata
mtaji huo kisha anza kuweka akiba.
à Hakikisha
unakuwa na nidhamu ya fedha, epuka kuitumia hiyo akiba.
“Haba na haba
hujaza kibaba”-Usidharau akiba ndogo unayoweka
0 Maoni