NAMNA YA KUZIFAHAMU FURSA (KNOWING AN OPPORTUNITIES)

Faraja Gasto
+255767955334

Fursa ni nini? (what an opportunity means)
Fursa ni kile ambacho unaweza ukakitumia na ukapata faida au ukatatua changamoto fulani hususani ya kiuchumi. Nimesema hususani ya kiuchumi maana ninafundisha ujasiriamali na biashara.

Ukweli ni kwamba
Kila mtu huwa anaona fursa ila shida iko kwenye KUFAHAMU KAMA HII NI FURSA.

MAMBO KADHAA YANAVYOTENGENEZA FURSA.
Yafuatayo ni mambo baadhi (sijayataja yote) yanayotengeneza fursa ambazo watu wanaziona na kuzitumia.

1.Matatizo ya watu na mahitaji ya watu
Kwa mfano kuna watu kutokana na masuala ya afya wamezuiwa kula vyakula fulani kisha wakaambiwa vyakula wanavyotakiwa kula, ukianza baishara ya kuuza hivyo vyakula  katika eneo hilo lazima upate wateja.
Kwa mfano kuna mahitaji ambayo ni ya lazima ambayo mwanadamu hawezi kuepuka nayo kwa mfano chakula, mavazi na malazi, hakuna ambaye hawezi kununua chakula, hakuna ambaye hawezi kunua mavazi n.k na pia kuna huduma ambazo zinahitajika kila mahali kwa mfano huduma ya afya (maduka ya madawa, hospitali na maabara), hizi biashara unaweza ukazifanya mahali popote maadamu watu wapo.

2.Matatizo yaliyopo kwenye eneo
Kwa mfano kama mahali fulani kuna tatizo la maji basi hiyo ni fursa, kama mahali fulani watu wananunua bidhaa mbali na mahali walipo hiyo ni fursa.

3.Taasisi zilizopo katika eneo fulani
Kwa mfano kama mahali fulani kuna shule au chuo au kanisa au msikiti n.k hiyo ni fursa, kwa mfano ukiweka mgahawa karibu na taasisi hizo lazima utapata wateja.
Kwa mfano ukitembelea mahali vilipo vyuo, utakuta kuna biashara za aina nyingi sana, hizo biashara zipo kwa sababu hizo taasisi zipo, ukitaka hizo biashara zifungwe fanya mchakato wa kuondoa hizo taasisi ghafla utaona watu wanafunga hizo biashara.

4.Miundombinu (infrastructures)
Kwa mfano barabara, miundombinu ya umeme n.k hizo huwa zinatengeneza fursa. Kwa mfano wapo watu ambao wanafanya biashara ya usafirishaji  kwa sababu barabara zipo, wengine wanafanya biashara ya usafirishaji wa anga, wengine wanafanya biashara ya usafirishaji wa majini. Hizo fursa zimetengenezwa na miundombinu mizuri.

5.Uwepo wa bidhaa
Bidhaa zote zimeganyika katika makundi makuu mawili;
1.Bidhaa zinazotokana na KILIMO (Agricultural activities)
Wataalamu wa kilimo wanatafsiri ufugaji ni shughuli mojawapo inayochuliwa kama shughuli ya kilimo, zipo bidhaa nyingi zinazozalishwa na shughuli za kilimo; matunda, mbogamboga, nafaka, ngozi n.k

2.Bidhaa zinazotokana na UZALISHAJI (Manufacturing)
Hizi ni bidhaa za viwandani; madaftari, kalamu, vyombo vya moto, vifaa vya kielektroniki n.k

3.Bidhaa zilizomo kwenye maji
Kwa mfano samaki n.k

4.Bidhaa zilizopo kwenye ardhi
Kwa mfano madini n.k

6.Uwepo wa ardhi yenye rutuba (fertile soil)
Ardhi yenye rutuba ndio inawafanya watu wajihusishe na shughuli za kilimo.
àMambo mengine yanayotengeneza fursa ni UTANDAWAZI, DINI, SIASA n.k. japo katika fundisho hili sijaeleza kuhusu jinsi hayo mambo yanavyotengeneza fursa.

NAMNA YA KUZIFAHAMU FURSA
Kama anilivyotangulia kusema kwamba kila mtu anaziona fursa ila shida iko kwenye KUFAHAMU KAMA HII NI FURSA ndio maana kichwa cha kipengele hiki nimesema ni “namna ya KUZIFAHAMU FURSA”
1.Hudhuria kwenye mafundisho ya ujasiriamali na biashara
2.Penda kufuatilia taarifa, midahalo na makongamano yanayohusu biashara na ujasiriamali

3.Penda kubadilishana mawazo na watu wengine kuhusu masuala ya biashara.

Chapisha Maoni

1 Maoni