UMUHIMU WA KUFANYA TATHMINI KATIKA KANISA


Na. Faraja Gasto

Bwana Asifiwe!!!

Ni makanisa machache sana ambayo huwa yanafanya tathmini kuhusu mwenendo mzima wa kanisa husika hususani katika kufahamu
1.Utendaji kazi wa kanisa na idara zake

2.Mafanikio na changamoto za kanisa

3.Hali ya kiroho ya washirika

4.Hali ya kimwili ya washirika

N. K   N. K

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya tathmini angalau kila baada ya miezi miwili.

UMUHIMU WA KUFANYA TATHMINI
1.Itasaidia kujua ni eneo gani linahitaji kushughulikiwa ili idara fulani ifanye kazi kwa weledi,  ili waumini wapende maombi n. K

2.Itasaidia kuandaa mipango mikakati ya kanisa kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali kwa kuwa tayari kutakuwepo na mwanga wa kutosha hususani wapi pa kuanzia na nini kiongezwe katika eneo fulani n. K

3.Itasaidia Wana maombi kujua ni mambo gani ya kuombea kulingana na hali halisi ilivyo.
Kwa kuwa kama wanamaombi watakosa kujua hali halisi ya kanisa watajikuta wanaombea vitu visivyo na umuhimu kwa wakati huo.

MAMBO YA KUTATHMINI YATAKAYOSAIDIA KUANDAA MIPANGO MIKAKATI YA KANISA

1.Mahudhurio ya Ibada na Maombi

2.Utoaji wa sadaka au Michango

3.Umoja wa viongozi

4.Je! Muda wa ibada unazingatiwa

5.Je! Kuna mtembeo wa nguvu za Mungu kanisani

6.Je! Waumini wanaongezeka au Hawaongezeki?

7.Hadhi ya ndoa ikoje: je! Wanawake wangapi ni wajane? Je! Wanawake wangapi wanasali na waume zao? Je! Wanawake wangapi wamume zao hawajaokoka? Je! Mwenendo wa ufungaji ndoa ukoje?(ndoa zinafungwa au la!)

8.Je! Kanisa lina malengo? Ipi Mikakati ya kufikia malengo hayo?

9.Je! Kuna Mikakati ya Kuinua huduma(vipawa) vya washirika? Je! Kuna Mikakati ya Kuinua Idara Mbalimbali? Kuinua hali za maisha ya waumini?

10.Je! Huduma tano zinatenda kazi kanisani? Je! Kuna udhihirisho wa Karama za Roho Mtakatifu?

11.Hali ya kanisa wakati linaanza na sasa ikoje(je! Kuna utofauti?)

12.Waumini wanafanya kazi zipi: Wamejiajiri au Wameajiriwa?

13.Muonekano wa waumini ukoje: wana afya?, Kuvaa Kwao kukoje? N.k

14.Kiwango cha Elimu Cha Waumini

15.Hali ya Makazi: Je! Waumini wangapi wamepanga na wangapi wamejenga? Je! Waumini Wanaishi kwenye nyumba za aina gani(je! Zina umeme, maji n.k? Je! Ni kubwa au ndogo? Je! Ni za block, tope au matofari choma?

16.Umbali wa kutoka kanisani mpaka kwenye makazi ya waumini ukoje? Je! Waumini wanafika kanisani kwa kutembea kwa mguu au wana vyombo vya usafiri?

17.Je! Kumbukumbu zipo? (idadi ya waumini, idadi ya waliompokea Yesu kwa kila mwaka)

18.Je! Kanisa linaweka juhudi katika suala la kuhubiri injili ambalo ndilo agizo la Yesu?  Au kanisa linaweka Juhudi katika kuanzisha miradi ambayo haiwaleti watu kwa Yesu?

N. B Sipingi suala la kanisa kuanzisha miradi ila ni muhimu tukumbuke Yesu hakutuambia kuanzisha miradi ila kama tunaanzisha miradi ni muhimu tukumbuke pia kuanzisha miradi inayolenga kuwaleta watu kwa Yesu.

----Hayo ni mambo ya msingi ya kuyafanyia tathmini kabla ya kuandaa mipango mikakati ya kanisa.

Chapisha Maoni

1 Maoni