Na. Faraja Gasto
Utangulizi
Watu wengi wamejikuta wakiharibikiwa kwa sababu ya kutendea kazi taarifa za kuambiwa ambazo hawana uhakika nazo.
Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya taarifa za kuambiwa, utasikia "ooh mume wako ana nyumba ndogo" "ooh mke wako ana mazoea na muuza duka" n. K kumbe taarifa hizo ni za uongo. Watu wengi pasipo kupambanua wamejikuta wakiumiza wake zao au waume zao kwa sababu ya taarifa za kuambiwa.
Kijana mmoja akaambiwa na mama yake "ooh siku hizi mke wako haniheshimu" yule kijana katoka na hasira akaenda kumpiga mkewe kumbe zilikuwa taarifa za uongo.
Nakusihi "JIHADHARI NA MANENO YA KUAMBIWA"
(mwanzo 39:1-20)
Ukisoma hilo andiko utawaona wahusika wakuu watatu
1.Potifa(Bosi wa Yusufu
2.Mke wa potifa
3.Yusufu (mfanyakazi)
Biblia inasema nyumba ya Potifa ilibarikiwa KWA AJILI YA YUSUFU"
siku moja mkewe akaleta kizaazaa, akamtamani mfanyakazi wao(Yusufu) akamwambia "LALA NA MIMI" lakini Yusufu akakataa, kitendo cha kukataa hakikumfurahisha huyo mama, siku moja Yusufu alipokuwa akifanya kazi, yule mama akamshika Yusufu kwa nguvu, lakini Yusufu akakataa akakimbia huku akiacha nguo yake mikononi mwa mke wa bosi wake.
*Mwanzo wa Kesi*
Mke wa bosi Wake akamsubiria mumewe akabadilisha maneno, akambambikizia kesi Yusufu kuwa alitaka kumbaka, Potifa kwa hasira akamshika Yusufu akamtia gerezani kwa sababu ya maneno ya kuambiwa.
Kumbuka nyumba yake ilibarikiwa kwa sababu ya uwepo wa Yusufu, kwa hiyo kitendo cha kumfunga Yusufu ilikuwa ni sawa na KUFUKUZA BARAKA ZITOKE NYUMBANI KWAKE.
Potifa alifanya maamuzi kwa hasira kwa sababu ALIPEWA TAARIFA AMBAZO KWA NJE ZILIONEKANA NI ZA UKWELI LAKINI kumbe zilikuwa za uongo.
N. B Shetani huwa ana tabia ya kutengeneza uongo na akatengeneza na ushahidi wa kusindikiza huo uongo, kama alivyofanya kwa Yusufu alitengenezewa uongo na ushahidi ukapatikana wa kusindikiza uongo.
(1Timotheo 5:22)
Biblia inasema "Usimwekee mtu mikono kwa haraka, usizishiriki dhambi za wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi"
Biblia inaposema "Usimuwekee mtu mikono kwa haraka" maana yake ni kwamba usiunge mkono hoja ya mtu, wazo la mtu n.k kwa haraka kwa kuwa haraka itakufanya ushiriki dhambi za wengine bila wewe kujua.
Hata kama umesikia taarifa fulani na zimetolewa na ushahidi usiwahi kutoa maamuzi, ni muhimu kutafakari kwanza ili utoke na maamuzi sahihi.
SWALI NILILOWAHI KUULIZWA WAKATI NILIPOFUNDISHA SOMO HILI SEHEMU FULANI.
Mama mmoja akaniuliza "ikiwa nimewasikia watu kwa masikio yangu wananisema, Nifanyeje? Je! Nikiwafuata nitakuwa nimekosea?
JIBU: Nikamwambia shida sio kuwafuata, shida ni UTAKATIFU WAKO, nikamwambia Je! Ukiwafuata wakakana hawajakusema wewe utapigana au?
Kwa hiyo ni muhimu kuomba Mungu akupe hekima ya kufanya juu ya hilo kwa kuwa unaweza kuwafuata na ukajikuta umewasha moto mwingine.
mungu akubariki kwa kujifunza, waweza kumshirikisha mwingine ili asije akajikuta amefanya maamuzi yasiyo sahihi kutokana na taarifa za kuambiwa.
0 Maoni