Mwl. Faraja Gasto
Bwana Yesu Asifiwe, hii ikiwa ni sehemu ya tatu ya somo, nahitaji niende moja kwa moja kwenye njia ya tatu ambayo Mungu anaitumia kumtaarifu mtu ni hii
(3)Mungu huwa anawatumia manabii au watumishi wake ambao si manabii
----Soma ushuhuda huu
>>>>Dada mmoja alinitumia ujumbe akitaka nimtafsirie ndoto aliyoota, aliponisimulia ile ndoto mpaka mwisho, Roho Mtakatifu akanipa swali la kumuuliza, nikamuuliza Je! Umepanga kusafiri kwenda sehemu fulani akajibu ndiyo, nikamwambia tafsiri ya ndoto yako ni hii "usiende huko unakotaka kwenda"
---Roho Mtakatifu alinitumia kumpa taarifa kwa kuwa ile safari aliyoipanga ingekuwa na madhara kwake kama angeenda.

(Matendo ya mitume 21:7-11)
Ukisoma andiko hilo utaona Roho Mtakatifu alimtuma Nabii kwa Mtume Paulo ili kumjulisha kuwa ikiwa atathubutu kwenda Yerusalemu basi atafungwa kwa kuwa kuna watu walikuwa wanakusudia mabaya juu yake, hiyo ilikuwa ni taarifa ya tahadhari juu ya mpango mbaya uliokusudiwa juu ya Mtume Paulo, lakini tunaona Mtume Paulo alilazimisha kwenda na alikumbana na shida kubwa sana.
Ninachotaka uone ni kwamba Kuna wakati Mungu huwa anatuma Nabii aende kwa mtu ili ampe taarifa za namna hiyo ili kumuepusha mtu huyo na hatari, ajabu ni kwamba katika nyakati za leo watu hawaamini kama manabii wapo, ila ni vema ufahamu manabii wapo na Mungu anawatumia, japo kuna manabii wa uongo wengi kwa nyakati hizi lakini na manabii wa ukweli wapo pia na kwa kuwa sizungumzii kumtambua nabii wa kweli au uongo nipende kukurudisha kwenye mada, njia ya kutuma manabii Mungu anaitumia mpaka leo kwa hiyo usije ukatweza unabii mwishowe ukajikuta umeharibikiwa.

Barikiwa, mshirikishe na mwingine
0 Maoni