Mwl.Faraja Gasto
Lengo la somo:Kukupa ufahamu ili unapoomba Mungu akuondolee vikwazo uwe unaelewa kanuni ambazo Mungu anazitumia kuondoa vikwazo.
UTANGULIZI
Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na upinzani katika kazi zetu, huduma zetu na maisha yetu kwa ujumla na kutokana na vikwazo tunavyokutana navyo wengine hukata tamaa na wengine humuomba Mungu amuondolee vikwazo kwa kuwa kila mtu hupenda kuona kila alichopanga kinafanyika kama alivyokusudia.
MGAWANYIKO WA VIKWAZO
1.Watu
Kuna watu katika maisha yetu huwa ni kikwazo kwa maono yetu n.k tena si ajabu wakawa watu wa karibu nasi(ndg, wazaz,watu unaowaheshimu n.k)
--Hata Yesu aliwahi kukutana na vikwazo tena ikafika hatua shetani akamtumia Petro ili awe kikwazo kwa Yesu(Mathayo 16:23)
2.Mazingira
Mazingira ynaweza kuwa kikwazo kwetu, shetani wakati mwingine huwa anayatumia mazingira kuweka vikwazo kwetu.
--Kuta za Yeriko zilikuwa kikwazo kwa wana wa Israeli katika safari yao ya kwenda kanaani lakini Mungu aliziangusha kuta za Yeriko(Yoshua 6:20)
3.Hali mbalimbali
Kuna hali kama ugonjwa, umaskini, kukata tamaa n.k huwa zinainuka ili kuwa vikwazo, kumbuka shetani hutengeneza hali hizo ili kutuzuia tusifike mahali fulani, shetani aliiachilia hali ya kutokuamini kwa wapelelezi kumi ili hali hiyo ihamie kwa wana wa Israeli na hatimaye wasiendelee na safari ya kwenda kanaani(Hesabu 13:32-33)(Hesabu 14:1-4)
FAHAMU HILI
Hakuna kikwazo ambacho Mungu kinamshinda Mungu kuondoa kwa hiyo si vema kukata tamaa kwa kuwa watu, hali au mazingira hayawezi kumzuia Mungu asifanye anachotaka.
KANUNI AMBAZO MUNGU ANAZITUMIA KUMUONDOLEA MTU VIKWAZO
1.Kuna wakati Mungu huwa ANATAMKA NENO LITAKALOONDOA HICHO KIKWAZO
(Zekaria 4:6-7)
Ukisoma hiyo habari utaona katika ulimwengu wa roho, shetani aliweka kikwazo kwa ajili ya mtumishi wa Mungu Zerubabeli na Zerubabeli hakujua kuwa kuna kikwazo amewekewa, Biblia inaonyesha alijitahidi kupambana na hali iliyokuwa kikwazo kwake bila mafanikio nduo maana Bwana akwamwambi "SI KWA UWEZO WALA SI KWA NGUVU BALI KWA ROHO WA BWANA" maana yake ni kwamba kile kikwazo kisingeondoka kwa jitihada zake bali kwa msaada wa Roho wa Bwana, baada ya hapo Bwana ALITAMKA NENO JUU YA KILE KIKWAZO ndipo kiliondoka.
Jiulize:Ni mara ngapi umejitahidi kupambana kwa uwezo wako ili kuondoa vikwazo vinavyokukabili?
---Ni vema ujifunze kumuomba Mungu aseme neno juu ya vikwazo vinavyokukabili.
2.Mungu huwa kuna wakati ANAKWENDA MBELE YA MTU ILI KUMSAWAZISHIA NJIA NA KUONDOA VIKWAZO
(Isaya 45:1-2)
Biblia inasema Mfalme Koreshi alijikuta anakabiliana na vikwazo na hakujua kwenye ulimwengu wa roho amewekewa vikwazo ili asifanye kile ambacho Mungu anamtaka afanye ndipo Bwana alipomwambia "NITAKWENDA MBELE YAKO ILI KUPASAWAZISHA MAHALI PALIPOPARUZA NA KUVUNJA MALANGO YA SHABA NA PINGO ZA CHUMA.
3.Mungu huwa kuna wakati ANAMFUNDISHA MTU NAMNA YA KUKABILIANA NA VIKWAZO.
(Yoshua 6:1-20)
Bwana aliwafundisha wana wa Israeli namna ya ambavyo ukuta wa Yeriko utavunjika ili waendelee na safari na walipofanya kama Mungu alivyowafundisha ndipo ukuta ulianguka.
(Kutoka 14:15-16)
Bwana alimfundisha Musa namna ya kutumia fimbo ili wapite katikati ya kikwazo ambacho Bahari ya shamu.
----Ni vema ufahamu Mungu anaweza akakupitisha katikati ya vikwazo hata kama vipo na ukapota katikati ya vikwazo na visiwe na uwezo wa kukuzuia.
Ila ni muhimu kujifunza kukaa na kumsikiliza Mungu.
*Utashinda na zaidi ya kushinda.*
0 Maoni