Mwl.Faraja Gasto
UTANGULIZI
Kila mwanadamu huwa ana mapendeleo yake(preferences) yaani kila mtu mtu huwa kuna vitu huwa anavipenda na kuna vitu huwa havipendi kutegemeana na sababu mbalimbali.
Watu wengi kutokana na tabia ya kukataa vitu bila kutafakari wamejikuta wakipoteza vitu vya maingi na vya muhimu katika maisha yao, watu wengi wamejikuta wakipoteza fursa na neema mbalimbali kutokana na tabia ya kukataa vitu bila kutafakari.
Unaweza ukaniuliza una maanisha nini? ili unielewe soma mifano hii iliyo katika mfumo wa maandiko.
(YOHANA 1:11,12&17)
Biblia inasema Yesu alikuja kwake(Israeli) lakini walio wake(wana wa Israeli) HAWAKUMPOKEA/HAWAKUMKUBALI(WALIMKATAA) lakini hawakujua kitendo cha kumkataa Yesu walikuwa wamekataa vitu vingi na vya muhimu alivyokuwa navyo Yesu, kwa mfano Uzima, Neema na kweli n.k
--Hivyo vyote walivikosa kwa kuwa HAWAKUMKUBALI, lakini wale WALIOMKUBALI walipata kitu kikubwa sana ambacho ni UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU.
Jiulize:Ni watu wangapi Mungu amekuletea na ukawakataa kwa sababu mbalimbali?
(MITHALI 31:10)
Watu wengi hususani vijana huwa wanaomba Mungu awape WAKE WEMA NA WAUME WEMA, lakini kutokana na tabia ya KUKATAA wengine wamejikuta wakikosa wake wema na waume wema na hatimaye wengine wamejikuta wakiolewa au wakioa mtu yeyote tu.
---Nataka niwatafakarishe vijana, Mungu anaweza akakupa mumue mwema na mke mwema na huyo mtu akaja kwako katika namna usiyotarajia, unapopoga picha ya nje unaweza kumkataa lakini kumbe ndiye mume au mke mwema, Kumbuka Mungu haangalii kama sisi wanadamu bali Mungu anaangalia ndani na Mungu anapokupa anakuwa ameangalia ndani lakini vijana wengi huwa wanaanglia mambo ya kimwili (sex body, handsome, beautiful , public figure n.k) na wengi wao wamejikuta wakikosa wake wema na waume wema kwa tabia ya KUKATAA BILA KUTAFAKARI, ni vema uelewe Mungu hatakushushia mume au mke mwema bali Mungu ATAKUPA na akikupa usipokuwa na ufahamu ndani yako utajikuta umekataa kitu cha Mungu kutokana na mitazamo na hisia mbovu.
Biblia inauliza "mke mwema ni nani awezaye kumuona? Maana yake ni kwamba kiuhalisia ni vigumu kupambanua kitu chema kwa kuwa unahitaji ufahamu wa kiungu(divine understanding) ili umuelewe Mungu.
Ndio maana nakuambia kabla hujamkataa mtu TAFAKARI kwa namna ya kiungu, ili usije ukakosa kitu cha Mungu.
*Mkikubali na Kutii mtakula mema ya nchi.*
0 Maoni