JINSI AMBAVYO MUNGU ANAPIMA UBORA WA SADAKA INAYOTOLEWA KWAKE

Mwl.Faraja Gasto

Bwana Yesu asifiwe!!!

Suala la utoaji wa sadaka limekuwa likileta utata kwa kanisa la leo kutokana na wingi wa mafundisho ambayo kimsingi mengine hayako sawasawa na neno la Mjngu, wengine wamehubiriwa kuwa sadaka yenye kibali kwa Mungu ni ile inayokuumiza moyo, jambo ambalo sio kweli kwa mujibu wa mandiko.

Ndio maana ninakuletea somo hili ili upate ufahamu ambao utakuwa msingi wa utoaji ulio sawasawa na neno la Mungu.

FAHAMU HILI
Ukubwa wa sadaka au wingi wa sadaka haumfanyi Mungu apokee hiyo sadaka bali kinachomfanya Mungu apokee sadaka ya mtu ni UBORA uliomo ndani ya sadaka hiyo bila kujali wingi au ukubwa wa sadaka.

SADAKA YENYE UBORA NI IPI?
1.Sadaka iliyotolewa kwa imani
(Waebrania 11:4)
--Biblia inasema KWA IMANI Habili ALIMTOLEA MUNGU dhabihu iliyo BORA, Biblia inataka tujue kuwa sadaka ili iwe na ubora lazima itolewe kwa imani, Mungu anapoona sadaka iliyotolewa kwa imani huwa anaihesabu hiyo sadaka kuwa ni sadaka yenye ubora unaostahili haijalishi sadaka hiyo ni kubwa au ndogo.

2.Sadaka iliyotolewa kwa moyo mkunjufu au moyo wa kupenda
(2Wakorintho 9:7)
Biblia inasema Mungu huwa anapenda mtu anayetoa kwa MOYO MKUNJUFU, sadaka iliyotolewa kwa moyo mkunjufu au moyo wa kupenda huwa ni sadaka yenye ubora, lakini endapo mtu atatoa ili aonekane kwa watu kuwa ametoa sadaka kubwa au mtu ambaye atatoa sadaka kwa kulazimishwa ilihali moyo wake unaumia ni vema aelewe sadaka hiyo itakuwa haina kibali kwa Mungu na sadaka hiyo itakuwa imepotea na haitaleta matokeo kwenye maisha ya mtu.

Hivyo ndivyo Mungu anavyotathmini kabla hajaipa sadaka kiwango cha ubora.

Mungu akubariki.

Chapisha Maoni

0 Maoni