USISIKILIZE SAUTI YA MAZINGIRA SIKILIZA SAUTI YA NENO




Utangulizi
Bwana Yesu asifiwe!!!!!
Napenda kukuletea somo hili ili kukufanya uinue imani yako katika kiwango kitakachokufanya upokee itu ktoka kwa Mungu maana mtu asiye na imani asidhani kuwa atapokea kitu kutoka kwa Mungu (Yakobo 1:6-7)
àMazingira yana sauti na neno la Mungu lina sauti na vyote hivyo huwa vinahitaji mtu avisikilize, watu wengi hujiukuta wakisikiliza sana kile ambacho mazingira yanasema kuliko kile ambacho neno linasema juu ya mazingira Fulani.
Kwa mfano mazingira yanaweza kukuambia kuwa utashindwa lakini neno la Mungu linakuambia tunashinda na zaidi ya kushinda.
Mazingira yanaweza kukuambia kuwa kuwa kwa kuwa kizazi kimetolewa basi huwezi kuzaa lakini wakati huohuo neno la Mungu lanakuambia kuwa yote yanawezekana kwake aaminiye.
àNinachotaka uone hapo ni kwamba mazingira huwa yanakinzana na neno la Mungu kwa hiyo ndio maana neo la Mungu linatuambia tusiviangalie vinavyoonekana bali visivyoonekana.

MADHARA YA KUSIKILIZA SAUTI YA MAZINGIRA
1.Hofu itaumbika ndani yako
àJaribu kufikiri mtu ambaye ameambiwa na Daktari kuwa ajikabidhi kwa Mungu kwa kuwa anakwenda kufa, mtu huyo akiangalia hayo mazingira na akayapokea ndani ya moyo wake lazima atajikuta amekufa kwa kuwa kitakachomuua sio ugonjwa bali ni hofu inayotokana na kile alichoambiwa na Daktari.

2.Utakosea katika kufanya maamuzi
àWatu wengi wamejikuta wakifanya maamuzi mabaya kwa kusikiliza sauti ya mazingira, kwa mfano maandiko yanasema kuwa “mwenye kuuangalia upepo hatapanda mbegu” (Mhubiri 11:4) kwa sababu amesikiliza mazingira lazima atajikuta anakosea katika kufanya maamuzi kwa kuwa mwenye kuangalia kile ambacho mazingira yanakuambia utajikuta kuna vitu hauvifanyi katika wakati unaotakiwa kuvifanya .

Chapisha Maoni

0 Maoni