Huwezi ukatenganisha
mafanikio na suala la kuamini kwa kuwa kila aliyefanikiwa kuna kitu alikiamini na
anaendelea kukiamini haijalishi ni cha kiungu au cha kishetani.
Biblia inasema kuwa imani
ni kuwa ni hakika ya mambo yatarajiwayo nan i bayana ya mambo yasiyoonekana (Waebrania
11:1).
Ni vema kila mtu ajue kuwa
kila mtu ambaye amefanikiwa aliamini jambo Fulani na akaingia kutendea kazi
kile alichokiamini na hatimaye akafanikiwa, nawe unapohitaji kufanikiwa katika
jambo lolote lazima uamini kwanza kuwa hilo jambo utaliweza na kama hauamini
kuwa utaliweza hilo jambo hata ufanyeje hautaliweza kamwe kwa kuwa “aonavyo mtu
nafsini mwake ndivyo alivyo” kwa hiyo kushinda au kushindwa huwa hakuanzii
kwenye mazingira ya nje bali huwa kunaanzia ndani ya mtu; anaamini nini,
anawaza, anakiri nini na anatenda nini.
Imani yoyote haijalishi ni
imani kwa Mungu au kwa shetani inajengwa na mambo makuu matatu (Warumi
10:17)
1.Kusika
2.Neno
3.Aliyesema hilo neno
Kwa hiyo ikiwa unahitaji
kufanikiwa katika jambo lolote lazima ujifunze kwa Mungu pekee kwa kuwa Baraka
zake zinatajirisha wala hazijachanganywa na huzuni ndani yake, lazima usikie
neno la Mungu linasema nini juu ya hicho kitu unachotaka kukifanya na pia
lazima utendee kazi hilo neno ulilosikia.
Kwa
nini uishi kwa imani?
1.Imani
ina uwezo wa kuamua ufanye jambo au mambo kwa viwango gani
Je! unataka kila
unachokifanya kifanyike katika ubora wa hali ya juu?
Ikiwa umejibu ndio katika
hilo swali soma biblia yako kwenye kitabu cha (Waebrania 11:4) ukisoma
andiko hilo utaona kuwa kwa imani
Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo
bora.
Biblia inataka ufahamu
kuwa imani iliyokuwemo ndani ya Habili ndio iliyoifanya sadaka yake ikawa bora
mbele za Mungu kwa hiyo kwa andiko hilo tunapata kujua kuwa imani itakufanya
ufanye mambo katika ubora.
2.Imani
inaweza ikakufanya ukawazidi waliokutangulia au wanaokuzudi
(Waebrania 11:4) ukisoma
andiko hilo utaona kuwa Habili alimzidi Kaini kwenye ubora, Kumbuka Kaini ndiye
kaka wa Habili na uwe na uhakika kuwa Kaini alianza kumiliki mali kabla ya Habili
lakini walipokwenda mbele za Mungu Habili alimzidi Kaini ubora japo wote
walitoa lakini ubora ulizidiana.
Nataka nikupe changamoto
hususani kama unafanya biashara, mnaweza mkawa mnafanya biashara ya aina moja
na kwenye eneo moja wewe na watu wengine lakini ambaye bidhaa yake itaonekana
kuwa na ubora kuliko nyingine ndio bidhaa itakayonunuliwa, ninachotaka ujue ni
kwamba kazi mojawapo ya imani ni kuweka ubora kwenye kila ambacho unakifanya
hata kama ni kidogo kiasi gani.
3.Imani inaweza ikakuhamisha(ikakuinua)
kutoka hapo ulipo na kukupeleka eneo lingine
(Waebrania 11:5)
Biblia inasema kuwa imani
aliyokuwa nayo Henoko ilimfanya Mungu amuhamishe ili asije akafa, kwa hiyo kwa
andiko hilo tunapata kujua kuwa imani inaweza ikakufanya utoke eneo moja kwenda
lingine.
0 Maoni