Kamusi
Oxford ya Kiswahili sanifu toleo la pili la Juni 2004 inasema siasa ni itikadi
inayofuatwa na kundi au jamii ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni
na mwenendo mzima wa maisha ya jamii hiyo au siasa ni mbinu ya utekelezajiau
uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo
linalotarajiwa.
Kamusi
kibindoni ya Kiswahili ya mwaka 2011 inasema siasa ni shughuli za serikali,
wanachama asasi za kutunga sheria au watu wanaojaribu kufanya maamuzi kuhusiana
na jinsi nchi inavyotawaliwa na pia siasa ni mkakati wa uendeshaji wa jambo kwa
kutumia busara na hekima.
0 Maoni